Miss Tanzania Photogenic 2014, Evelyn Baasa.
Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Redd’s Miss Tanzania
Photogenic 2014, wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa taji hilo, Evelyn Baasa
(katiakti) jana. Wengine kutoka kushoto ni Nicole Sarakikya, Lilian Kamazima,
Lilian Timothy na Dorice Mollel.
Warembo wakilisakata rumba kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo.
Baadhi ya warembo wakipiga picha ya pamoja na mshindi huyo wa Taji la Miss Tanzania
Photogenic 2014 MlimbwendeEvelyn Baasa (19) jana aliibuka kidedea kati ya walimbwende
wenzake 30 na kutwaa taji la Redds Miss Photogenic 2014.Kwa kushinda taji hilo Baasa
ambaye alinzania mbio za taji la Miss Tanzania katika Kitongoji cha Karatu naabadae
kuingia Miss Arusha na Kanda ya Kaskazini amekuwa mrembo wa kwanza kuingia
Nusu Fainali ya mashindano Miss Tanzania 2014. Shindano hilo ni moja kati ya mataji
matano ambayo yanashindaniwa na warembo hao ambapo washindi wake wanapata tiketi
ya kuingia Nusu Fainali ya shindano hilo litakalo fanyika mapema mwezi ujao.
Miongoni mwa mataji hayo ni Miss Tanzania Photogenic, Miss Tanzania Top Model,
Miss Tanzania Personality, Miss Tanzania Sports Lady na Miss Tanzania Talent.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Lino International Agency, waandaaji wa Shindano la
Miss Tanzania, Hashim Lundenga ‘Uncle’ amesema jopo la majaji watatu ambao ni wapiga
picha na wadau wa masuala ya urembo wa masuala ya urembo Tanzania walikaa na
kumchagua mshindi huyo kupitia picha mbalimbali za warembo hao.
Majaji waliowezesha kupatikana kwa mshindi huyo ni Mpigapicha mkongwe wa masuala ya urembo nchini Mroki Mroki ambaye anafanyakazi na Magazeti ya Serikali ya Daily News na Habarileo,
Mtayarishaji wa vipindi Elliud Pemba wa True Vision na Afisa Itifaki Ofisi ya Mkuu
wa Mkoa Arusha, Mukhsin Kassim.
Taji la Redd’s Miss Tanzania Photogenic lilikuwa linashikiliwa na Redd’s Miss
Tanzania 2013 Happyness Watimanywa.Warembo wengine waliofanikiwa kuingia hatua
ya tano bora ya Miss Photogenic ni Dorice Mollel, Nicole Sarakikya, Lilian Timothy na
Lilian Kamazima. Kesho warembo hao watachuana tena kuwania taji la Miss Top Model
katika shindano litakalofanyika Triple A jijini Arusha.
Kutana na Miss Redds Tanzania Photogenic 2014 Evelyn Baasa
Reviewed by habari motto
on
3:03 PM
Rating: