Katika Bonanza hilo lililozishirikisha Timu nne lilifanyika jana katika viwanja vya Chuo cha Uhasibu Mbeya(TIA) zikiwmo timu kutoka Baa ya Kalembo ya Sokomatola, Tugelepo ya Mbata na wenyeji Wanafunzi wa TIA.
Timu ya Salalizya fc ya Mabatini ilijinyakulia zawadi ya Katoni 8 za Bia aina ya Serengeti baada ya kuishinda timu ya Wanafunzi wa TIA katika fainali kwa magoli mawili kwa nunge hivyo TIA kuibuka mshindi wa pili na kujinyakulia Katoni 4 za bia.
Awali timu ya Salalizya iliifunga Tugelepo goli moja kwa bila katika mchezo wa utangulizi na kasha timu ya TIA kuitoa timu ya Kalembo kwa mikwaju 9 kwa 8 baada ya muda wa kawaida kutofungana.
Mshindi wa tatu ilikuwa ni timu kutoka baa ya Kalembo baada ya kuifunga timu ya Tugelepo kwa mikwaju 4 kwa 2 ya penati katika kumtafuta mshindi wa tatu kutokana na kutoshana nguvu katika muda wa kawaida.
Hivyo Mshindi wa tatu alijipatia Katoni Mbili huku timu ya Tugeleo ikijipatia Katoni Moja kutokana na kuwa mshindi wa nne na wa mwisho.
Katika Bonanza hilo Mgeni rasmi aliyegawa zawadi kwa washindi alikuwa ni Mkurugenzi wa Hoteli ya Kimataifa ya PADZ iliyopo Forest Mpya, Patrick Zambi, ambaye alitoa wito kwa vijana kupenda michezo na kujikita katika mazoezi ili kuim,arisha afya zao.
Mwisho.
Na Mbeya yetu/Stanslaus Lambart