Erasto Nyoni Agonga Mtu,MADEREVA BODABODA WAMPIGA KAMA MWIZI


Beki wa Azam FC, Erasto Nyoni amekutwa na mkasa mkubwa baada ya kumgonga dereva bodaboda katika eneo la Tip Top Manzese lakini akaendelea kukimbia akiyagonga baadhi ya magari hadi katika eneo la Kijitonyama jijini Dar ambako alikwama baada ya kuligonga gari la Global Publishers.

Baada ya tukio hilo, Nyoni, beki wa Taifa Stars alitoka kwenye gari lake aina ya Toyota Grande Mark 11 GX 110, akaanza kujitahidi kukimbia kutokana na lundo la bodaboda kuanza kumfukuza wakitaka kuchukua sheria mkononi, hali iliyomtia hofu.
Walimfukuza hadi kufika eneo la Kijitonyama ambako alikwama baada ya kuligonga gari hilo la GPL na alipoteremka kwenye gari, wakaanza kumshambulia kama mwizi.
Nyoni alishambuliwa na lundo la madereva Bodaboda, lakini akafanikiwa kukimbia huku wakiendelea kumpiga na hata watu walipojitokeza kumsaidia, waliendelea kumpiga bila huruma.

Kwa mujibu wa walioshuhudia, Nyoni alishambuliwa kama mwizi katika eneo la tukio huku zaidi ya watu 30 wakimpiga.
 
Beki huyo wa Azam FC alionekana kama anakimbilia kituo cha Polisi cha Kijitonyama Mabatini, lakini hakufanya hivyo na madereva hao wa Bodaboda walipomnasa walikuwa wakimshambulia kama mwizi naye alijaribu kujitetea na alipozidiwa, alitokomea kusikojulikana.
 

GARI LA BEKI ERASTO NYONI WA AZAM FC (KULIA) LIKIWA KATIKA ENEO LA KIJITONYAMA BAADA YA KUKWAMA KUTOKANA NA KULIGONGA GARI LA GLOBAL PUBLISHERRS.
NYONI ALISHAMBULIWA KAMA MWIZI NA MADEREVA BODABODA AMBAO WALIMKIBIZA KUTOKA ENEO LA MANZESE TIP TOP WAKIMTUHUMU KUMGONGA MWENZAO HALAFU AKAGOMA KUSIMAMA. TAARIFA ZIMEELEZA, NYONI ALISHINDWA KUSIMAMA KUTOKANA NA HOFU YA KUPIGWA NA MADEREVA BODABODA HAO WALIOKUWA NA JAZBA KUPINDUKIA.

CHANZO: SALEHJEMBE BLOG.COM
Erasto Nyoni Agonga Mtu,MADEREVA BODABODA WAMPIGA KAMA MWIZI Erasto Nyoni Agonga Mtu,MADEREVA BODABODA WAMPIGA KAMA MWIZI Reviewed by habari motto on 10:18 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.