Shuhudia Jinsi Harusi Ya Nyani Ilivyofana


Zaidi ya wakazi 200 katika kijiji kimoja kaskazini mwa India wamehudhuria sherehe ya harusi ya nyani wawili. 
Harusi hiyo iliandaliwa na mmiliki wa nyani hao, ambaye alisema nyani dume ni kama "mwanaye".
Sherehe hiyo ilifanyika siku ya Jumatatu katika wilaya ya Bettiah, katika jimbo la Bihar, huku "bi harusi" akiwa amevalia gauni maridadi. 
Nyani ni viumbe wanaopendwa na watu wa jamii ya wa-Hindu.
"Bwana harusi" ambaye anajulikana kama Ramu pamoja na mkewe mpya aitwaye Ramdulari walipitishwa katika mitaa ya kijiji wakiwa juu ya gari lililopambwa kwa maua na muziki ukichezwa, huku mamia ya wanakijiji wakijipanga kuwashangilia.
Mmiliki wa nyani hao Udesh Mahto ambaye ana watoto watatu wa kiume amesema nyani Ramu ni kama mtoto wake wa kwanza.
Shuhudia Jinsi Harusi Ya Nyani Ilivyofana Shuhudia Jinsi Harusi Ya Nyani Ilivyofana Reviewed by habari motto on 10:28 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.