MbugeWa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono Alishwa Sumu


Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono amelishwa sumu
wakati akiwa kwenye safari ya kikazi jijini London nchini
Uingereza, imeelezwa.
Kwa mujibu wa tovuti ya The Citizen, Mkono ambaye pia ni
mwanasheria maarufu, aliugua ghafla alipokuwa jijini humo.
Madaktari wake walisema kuwa alikuwa amelishwa sumu
iliyokuwa imekusudiwa kuharibu figo zake ndani ya saa 72.
“Ilikuwa siku mbili tangu niwasili London, nilianguka wakati
nikifanya shughuli zilizonileta huku,” alisema na kuongeza:
“Nilijisikia vibaya na kupoteza kumbukumbu kwa takriban saa
sita.”
Imeelezwa kuwa mbunge huyo alianza kutokwa jasho jingi
ghafla kabla hajaanguka.
“Baada ya kuhudumiwa, madaktari wa London walisema sumu
ilikuwa inaharibu figo yangu,” alisema.
Kwa mujibu wa mbunge huyo, alikuwa ameonywa mapema
kuwa muda mfupi kabla hajasafiri kwenda London anapaswa
awe mwangalifu, pia asifikie kwenye hoteli zilizokuwa
zimeandaliwa kwa ajili ya kundi kutoka Tanzania, hivyo aliamua
kufikia kwenye makazi yake jijini humo.
“Nilipokea meseji mbili kutoka kwa baadhi ya marafiki zangu
wakinionya kuwa mwangalifu wakati wote,” alisema na
kuongeza kuwa: “Nilikuwa nimeongozana na baadhi ya
wabunge katika safari hiyo. Taarifa zinaeleza kuwa maofisa
usalama wa kikosi cha upelelezi nchini Uingereza wameanza
kulichunguza suala hilo.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema kuwa taarifa
kuhusu tukio hilo zilishafikishwa ofisi za Bunge ingawa hakuna
maelezo ya kutosha.
“Ninafahamu kuwa Mbunge Mkono alipata matatizo ya kiafya
wakati akiwa London, lakini anaendelea vizuri…maelezo
kuhusu ugonjwa wake unabaki siri kati ya Mkono na madaktari
wake,” alisema.
Mkono alikuwa mshauri mkuu wa Shirika la Umeme nchini
(Tanesco) na Serikali dhidi ya Kampuni ya Kufua Umeme ya
IPTL na kwamba aliwahi kuziwakilisha kwenye Mahakama ya
Kimataifa ya Utatuzi wa Migogoro ya Kibiashara (ICSID) kabla
ya mkataba wake kumalizika mwanzoni mwa mwaka huu.
Tanesco walikataa kusaini upya mkataba wa Mkono. Mbunge
huyo anatajwa kuwa nyuma ya kuvuja kwa kashfa ya Escrow,
kutokana na taarifa nyingi anazoweza kuwa anazifahamu
kuhusu sakata hilo.
Julai mwaka huu, Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter
Muhongo alimtuhumu Mkono kutumia kashfa ya Escrow
kumchafua, tuhuma ambazo Mkono anazikana.
Wiki chache baadaye, Spika alimtaka Mkono kueleza namna
ambavyo aliishughulikia kesi ya IPTL na Standard Chartered
Bank Hong Kong iliyokuwa imefunguliwa dhidi ya Tanesco na
Serikali.
Mkono aliwasilisha taarifa kuhusu kuchotwa kwa Sh207 bilioni
kwenye akaunti ya Escrow kutoka Benki Kuu ya Tanzania
wakati ambapo kulikuwa kuna kesi nyingine inaendelea kwenye
mahakama ya kimataifa.
Hatuwezi kuthibitisha kama kuna uhusiano wowote kati ya
kulishwa sumu na kashfa ya Escrow. Mkono amekuwa akisema
kuwa uchunguzi pekee ndiyo utakaoeleza ukweli
MbugeWa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono Alishwa Sumu MbugeWa Musoma Vijijini,  Nimrod  Mkono Alishwa Sumu Reviewed by habari motto on 1:46 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.