- Ballon d'Or: Cristiano Ronaldo
- MCHEZAJI BORA KWA WANAWAKE: Nadine Kessler
- TUZO YA PUSKAS: James Rodriguez
- KOCHA BORA DUNIANI: Joachim Low
- KOCHA BORA WANAWAKE: Ralf Kellermann
MSHAMBULIAJI wa Ureno, Cristiano Ronaldo ameshinda tena kwa mara ya pili mfululizo tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, Ballon d'O usiku huu mjini Zurich, Usiwsi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa 29 amewashinda Manuel Neuer wa Ujerumani na mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Argentina.
Ronaldo alitoa mchango mkubwa kwa Real Madrid kushinda mataji manne mwaka jana, akifunga mabao 56 katika mechi 51 vigogo hao wa Hispania wakisomba mataji ya Copa del Rey, Ligi ya Mabingwa, Super Cup ya UEFA na Klabu Bingwa ya Dunia
Cristiano Ronaldo akiwa ameshika tuzo yake Ballon usiku huu baada ya kukabidhiwa
Ronaldo (kushoto) akifurahia na mwanasoka wa kike wa Brazil, Marta
Pamoja na kutangazwa tuzo mbalimbali kwenye Ballon d’Or leo, pia kilitangazwa kikosi cha wachezaji 11 bora kwenye nafasi zote 11 uwanjani.
Mchezaji mmoja tu kutoka Ligi Kuu England ambaye ni Angelo Di Maria wa Manchester United ndiye alitajwa.
Wengine wanatokea katika klabu za Hispania, Ujerumani na Ufaransa huku Italia ikiambulia patupu.
World XI:
Neuer; Lahm, Ramos, David Luiz, Thiago Silva; Di Maria, Iniesta, Kroos; Messi, Ronaldo, Robben
ChristianoAmliza Tena Lionel Messi Atwaa Tuzo Mwanasoka Bora 2014
Reviewed by habari motto
on
12:52 PM
Rating: