Mashirika ya Kisomalia kuendelea na shughuli zao Kenya

Mfanyakazi wa benki ya Baraakat akiongea na mteja wa kisomalia
Mfanyakazi wa benki ya Baraakat akiongea na mteja wa kisomalia
 Baada ya Kenya kuyafungia mashirika ya Kisomali kuendelea na shughuli zao nchini humo mashirika ya misaada ya kibinadamu yameitaka Kenya kuruhusu mashirika ya kusafirisha fedha ya Kisomali kuanza tena shughuli zao ili kuwanusuru wakazi waishio Somalia.
 Taarifa iliyotolewa na mashirika kama Oxfam, CARE, Mercy Corps, Adeso na World Vision Somalia imesema kuwa familia za Kisomali zimepoteza njia pekee rasmi, ya wazi na yenye nidhamu inayotumiwa kutuma na kupokea fedha na kwamba mashirika yanayofanya kazi nchini Somalia pia yanakabiliwa na hatari ya kukosa njia pekee ya kusafirisha fedha kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za kibinadamu na operesheni za maendeleo nchini Somalia.
 Jumatano iliyopita serikali ya Kenya ilisimamisha vibali vya mashirika 13 ya kusafirisha fedha ya Kisomali yaliyoko mjini Nairobi katika juhudi za kuzuia fedha zisifikie kwa kundi la kigaidi la al Shabab.
 Hatua hiyo ilichukuliwa baada ya kundi hilo kuua watu wasiopungua 148 katika shambulizi lililolenga mabweni ya Chuo Kikuu cha Garissa huko mashariki mwa Kenya.
Mashirika ya Kisomalia kuendelea na shughuli zao Kenya Mashirika ya Kisomalia kuendelea na shughuli zao Kenya Reviewed by habari motto on 11:38 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.