June 29 2015 Burundi wanafanya Uchaguzi Mkuu leo, lakini ishu ni kwamba Uchaguzi huo wa Wabunge unafanyika huku vyama vya Upinzani wakiwa wamesusia Uchaguzi huo.. kingine ni kwamba japo kumekuwa na machafuko ya muda mrefu kupinga RaisPiere Nkurunziza kugombea kwa mara ya tatu kwenye Uchaguzi huo lakini Ratiba inavyoonesha ni kwamba Uchaguzi wa Rais utafanyika mwezi July 2015.
Leo umefanyika Uchaguzi wa Wabunge, picha zilizoenea Mitandaoni zinamwonesha Rais Nkurunziza akiwa anaelekea kupiga kura akitumia usafiri wa baiskeli.

Pembeni ya vituo vya Kupigia kura walikuwepo Askari wakiwa na silaha kuhakikisha Usalama unakuwepo.
Rais Nkurunziza alivyofika Kupiga kura kwenye Uchaguzi leo June 29 2015 Burundi.
Reviewed by habari motto
on
7:13 PM
Rating: