Chelsea jana iliendelea kukubali kipigo cha tatu mfululizo katika ligi na cha saba katika michezo 12 waliyocheza tangu kuanza kwa msimu huu baada ya kufungwa goli 1-0 kutoka kwa Stoke City katika uwanja wa Brittania.
Katika mchezo huo ambao kocha Jose Mourinho hakuwepo uwanjani, kutokana na adhabu aliyopewa wiki iliyopita ya kukaa nje ya uwanja kwa mechi moja, ilishuhudia Chelsea wakishindwa kabisa kuonesha nini wanataka.
Lakini pamoja na matokeo haya, ambayo yameifikisha Chelsea katika nafasi ya 16 huku wakikusanya points 11 katika michezo 12, golikipa Asmir Begovic anasisitiza kuwa wachezaji wote wanapigana kumsaidia kocha wao.
Kipa huyo ambaye anakaa golini hivi sasa tangu kuumia kwa golikipa namba moja wa timu hiyo Thibaut Courtois anasema kuwa, wachezaji wapo pamoja na Mourinho na kwamba ni mtu sahihi klabuni hapo.
Wakati huo huo, mchambuzi wa soka na mkongwe wa zamani wa klabu ya Newcastle na timu ya taifa ya England, Alan Shearer amesema kuwa pamoja na mambo mengine, Chelsea inatatizo kubwa na ushambuliaji msimu huu.
Begovich: “Wachezaji wote wa chelseatunamsapoti MOURINHO”
Reviewed by habari motto
on
9:55 AM
Rating: