Mshambuliaji Mtanzania wa Klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo DRC, Thomas Ulimwengu (kushoto) na mchezaji mwenzake raia wa Ghana, Solomon Asante (kiungo wa kati) wakishangilia baada ya kufunga timu ya USM Alger ya nchini Algeria.
Kombe la mshindi wa ligi ya mabingwa Afrika ambalo TP Mazembe wamelitwaa 2015.
Na Rabbi Hume
Klabu ya TP Mazembe ya nchini Congo DRC imetwaa kombe la ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuifunga timu ya USM Alger ya nchini Algeria kwa goli mbili (2) kwa bila na hivyo kuwa na utofauti wa goli nne kwa moja.
Magoli ya TP Mazembe yamefungwa na Mtanzania Mbwana Samata katika dakika ya 73 ya michezo huo na goli ya pili likifungwa na Roger Assale dakika ya 90 ya mchezo huo.
Baada ya kutwaa ubingwa huo unakuwa wa tano kwa timu hiyo, miaka waliyotwaa ubingwa huo ni 1968, 1969, 2009, 2010 na 2015.
TP Mazembe imetwaa ubingwa huo na hivyo kupata nafasi ya kuiwakilisha Afrika katika michuano kombe la Dunia la vilabu linalotarajiwa kufanyika Japan Desemba mwaka huu.
Katika mashindano hayo imeshuhudiwa kwa mara ya kwanza wachezaji kutoka Tanzania, Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wakitwaa ubingwa huo na Samata akiweka historia nyingine ya kuwa Mtanzania wa kwanza kutwaa tuzo ya mfungaji bora kwa kuwa na goli nane (8) na kumwacha Bakry ‘Al Medina’ Babiker anayechezea Al Merrick ya Sudan aliye na goli saba (7).
TP Mazembe yatwaa kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika
Reviewed by habari motto
on
7:22 AM
Rating: