Justin Bieber ashuka jukwaani kwa hasira

Staa wa muziki wa RnB na Pop, Justin Bieber haishiwi visa. Wakati wa tamasha Jumapili mjini Manchester, Uingereza aliondoka jukwaani na kutupa mic chini baada ya kuwataka mashabiki kutopiga kelele wakati akiimba.
rs_1024x759-161024092720-1024-justin-bieber-manchester
E-News iliripoti kuwa Justin aliawaonya mara ya kwanza mashabiki wasipige kelele wakati anaongea nao lakini hawakusikia. “Nashukuru sana kwa upendo wenu mnaouonyesha kwangu, hizi kelele tafadhali naomba ziachwe, ninashukuru tena lakini sidhani kama ni lazima kwenu kushangilia wakati naongea kwasababu najisikia kama nataka kuunganishwa na ninyi,” Justin aliwasihi mashabiki ambao hata hivyo hawakumsikiliza.
Lakini baadaye Bieber mwenye miaka 22 alirudi kuendelea na tamasha na kuelezea kwa nini aliondoka kwa hasira. “Nahisi kwamba nataka wasiliana nanyi.Lengo hapa ni ninapowaangalia katika macho mnajua kwamba tuko katika wakati muhimu na kwamba tunawasiliana,” alisema.
Justin Bieber ashuka jukwaani kwa hasira Justin Bieber ashuka jukwaani kwa hasira Reviewed by habari motto on 1:51 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.