Ivan Perisic (wa pili kulia)akipongezwa na wenzake baada ya kufungia timu
yake bao la pili.
KITENDO cha Alex Song kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Croatia, Mario
Mandzukic na kuoneshwa kadi nyekundu rasmi kimeua matumaini ya Cameroon kufuzu
hatua ya 16 ya kombe la dunia katika kundi A mjini mjini Manaus.
Song alishikwa na hasira dakika ya 40 na kufanya kitendo cha kinyama kwa
Mandzukic wakati huo Cameroon ikiwa nyuma kwa bao 1-0.
Baada ya Hispania kutupwa nje ya michuano, Cameroon imekuwa nchi ya
kwanza kwa Afrika kufangasha virago katika fainali za kombe la dunia mwaka huu
kutokana na kipigo kikubwa cha mabao 4-0 dhidi ya Croatia.
Kufuatia kadi nyekundu ya Song, mambo yalikwenda kombo zaidi na
kushuhudia Cameroon wakimalizia usiku vibaya baada ya kufungwa mabao matatu
kipindi cha pili na ndoto za kufuzu kuzimwa kabisa.
Hata hivyo kituko kikubwa ni beki wa Tottenham Benoit Assou-Ekotto
kuamua kupigana na mwenzake Benjamin Moukandjo katika hatua za mwisho za
mchezo huo.
Hapa chini ni vikosi vya wachezaji na viwango vyao.
Alama zimetolewa chini ya 10
Kikosi cha Cameroon: Itanjde 4.5; Mbia 4, Chedjou
4.5 (Nounkeu 46, 3), N’Koulou 4.5, Assou-Ekotto 5; Song 2, Matip 5, Enoh 5;
Moukandjo 4, Aboubakar 7 (Webo 70, 7), Choupo 6 (Salli 5).
Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Feudjou,
Djeugoue, N’Guemo, Eto’o, Makoun, Bedimo, Fabrice, Nyom, N’Djock.
Kadi nyekundu: Song.
Kikosi cha
Croatia: Croatia: Pletikosa 6; Srna 7.5,
Lovren 6, Corluka 6, Pranjic 7; Rakitic 7.5, Modric 7.5, Sammir 6.5 (Kovacic
70, 7); Perisic 8.5 (Rebic 78, 6), Mandzukic 7, Olic 8 (Eduardo 69, 7).
Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Zelenika, Vrsaljko, Vukojevic, Jelavic, Schildenfeld, Brozovic, Mocinic, Vida, Subasic.
Kadi ya njano: Eduardo.
Waliofunga magoli: Olic 11, Perisic 48, Mandzukic 61, 73
Idadi ya watazamaji: 36,000
Mwamuzi: Pedro Proenca (Portugal)
Mchezaji bora wa mechi: Ivan Perisic
Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Zelenika, Vrsaljko, Vukojevic, Jelavic, Schildenfeld, Brozovic, Mocinic, Vida, Subasic.
Kadi ya njano: Eduardo.
Waliofunga magoli: Olic 11, Perisic 48, Mandzukic 61, 73
Idadi ya watazamaji: 36,000
Mwamuzi: Pedro Proenca (Portugal)
Mchezaji bora wa mechi: Ivan Perisic
Kiungo wa zamani wa Arsenal man Alex Song alitolea nje kwa kadi
nyekundu.
Assou-Ekotto na Moukandjo walipigana
baada ya kipigo hicho
AMEROON
HOLAA! YAPIGWA 4-0 NA CROATIA, RASMI WAAGA MASHINDANO, WACHEZAJI
WAZIPIGA `LAIVU`… - See more at:
http://shaffihdauda.com/?p=2312#sthash.Xj64Qlvh.dpuf
CAMEROON WAAGA MASHINDANO,FULL TIME CAMEROON 0- 4 CROATIA
Reviewed by habari motto
on
8:30 AM
Rating:
