Waliofariki Kwa Corona Marekani Wafika 12,722

10:33 AM
Marekani imerekodi vifo vingi vya ugonjwa wa corona kwa siku huku watu 1,736 wakifariki siku ya Jumanne.

Idadi hiyo inaweka watu waliofariki kutokana na virusi hivyo nchini humo kufikia 12,722 kulingana na data za chuo kikuu cha Johns Hopkins.
Marekani ina wagonjwa 398,000 wa virusi hivyo waliothibitishwa , ikiwa ndio idadi kubwa zaidi duniani .
Wakati hayo yakijiri, Rais wa Marekani Trump ametishia kulikatia fedha shirika la afya Duniani WHO kwa sababu amesema shirika hilo halikutilia maanani kwa namna ilivyopasa hatari ya maambukizi ya virusi vya corona.
Trump amelilaumu shirika hilo kwa kuegemea zaidi upande wa China.  Rais huyo wa Marekani amedai kwamba asasi hiyo ya kimataifa ilishirikiana na China katika miezi kadhaa iliyopita kupuuza hatari ya maambukizi ya virusi vya corona.
Akitoa taarifa juu ya hali ya maambukizi hayo nchini Marekani, Trump alipuuza umuhimu wa taarifa ya mshauri mwandamizi iliyotolewa mapema mwaka huu kutahadharisha juu ya uwezekano wa kulipuka kwa maambukizi hayo. Rais huyo amedai kwamba hakuiona taarifa hiyo.
Badala yake Rais huyo wa Marekani amelishukia shirika la afya duniani WHO na kulitishia kulikatia fedha.Trump amesema asasi hiyo inaegemea sana upande wa China kuhusu mkakati wake wa kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.
Amedai kwamba Shirika la WHO lilishirikiana na China katika juhudi za nchi hiyo za kupunguza hatari ya mlipuko wa maambukizi hayo.
Rais Trump amesema Shirika hilo limeisifu China ingawa pana sababu ya kuwa na mashaka juu ya idadi rasmi  iliyotolewa na serikali ya China juu ya vifo vilivyotokana na mambukizi ya virusi vya corona
Waliofariki Kwa Corona Marekani Wafika 12,722 Waliofariki Kwa Corona Marekani Wafika 12,722 Reviewed by habari motto on 10:33 AM Rating: 5

Afrika Kusini yapiga marufuku raia wake kutoka nje

11:32 AM
Afrika Kusini imeanza kutekeleza leo amri ya watu kubakia majumbani mwao chini ya uangalizi wa jeshi, na kujiunga na nchi nyingine za Afrika zinazoweka hatua kali za watu kutotoka nje na kufunga shughuli nyingi katika jitihada za kusitisha kusambaa kwa virusi vya corona.

Watu milioni 60 nchini Afrika Kusini watalazimika kukaa nyumbani kwa siku 21.

Afrika Kusini ina visa 927 vya maambukizi ya virusi vinavyo sababisha ugonjwa hatari wa Covid-19 (Corona).

Hatua hizo zilitangazwa Jumatatu jioni na Rais Cyril Ramaphosa, ambaye alisema anataka kuzuia mlipuko wa janga la Covid-19 na kuepuka janga la kiafya.

"Kaeni nyumbani.... Baa, migahawa, maeneo ya starehe, mbuga, makanisa vimefungwa. Hakuna gari inyopaswa kutembea katika mitaa ya nchi hiyo.

"Maafisa pekee wanaofanya kazi katika sekta muhimu ndo ambao wanaruhusiwa kwenda kazini: hospitali, maduka ya dawa, maduka makubwa, maduka ya chakula. Watu wanaofanya kazi katika sekta za maji na umeme wanaweza pia kwenda kazi. Wafanya kazi katika sekta ya migodi ya makaa ya mawe, wataendelea kuripoti kazini.

"Ni marufuku mtu kutoka nje, barabarani, kwenda sehemu anakotaka," ameonya Waziri wa Polisi Mbeki Cele.
Afrika Kusini yapiga marufuku raia wake kutoka nje Afrika Kusini yapiga marufuku raia wake kutoka nje Reviewed by habari motto on 11:32 AM Rating: 5

Mo Salah achunguzwa

7:02 AM

Haki miliki ya picha

Related image
Mshambuliaji wa Liverpool raia wa Misri Mohamed Salah anachunguzwa na polisi baada ya video yake kuibuka akionekana kuendesha gari akiwa bado anatumia simu.
Klabu yake inadaiwa kuwa ndiyo iliyopiga simu kwa polisi.
Polisi wa Merseyside wamethibitisha kupitia ujumbe wa Twitter kwamba video hiyo imekabidhiwa kitengo husika.
Msemaji wa Liverpool amesema waliwafahamisha polisi kuhusu video hiyo baada ya kuzungumza na mchezaji huyo
Ameongeza kwamba hatua zozote zinazohitajia kuchukuliwa kuhusu tukio hilo zitachukuliwa kwa kufuata mifumo ya ndani.
Video hiyo ambayo imesambazwa sana kwenye Twitter inaonekana kumuonesha mchezaji huyo, akiwa anatumia simu yake akiwa amelisimamisha kwa muda huku akiwa amezingirwa na mashabiki, wakiwemo watoto. Kisha analingurumisha gari na kundoka akiwa bado anaitumia simu yake.

SalahHaki miliki ya picha
Image captionVideo hiyo inayodaiwa kumuonesha Mo Salah akiendesha gari akiwa bado anatumia simu imesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii

Msemaji wa klabu hiyo amesema: "Klabu, baada ya kushauriana na mchezaji, imewafahamisha Polisi wa Merseyside kuhusu kanda hiyo ya video na matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa kupigwa kwa video hiyo."
"Tumezungumza na mchezaji huyo na tutashughulikia hatua nyingine zozote zinazohitajika kuchukuliwa kwa kutumia mifumo ya ndani.
"Hakuna yeyote kati ya klabu na mchezaji ambaye atatoa taarifa zaidi kuhusu tukio hili."
Raia huyo wa Misri aliwafungia Liverpool magoli 44 msimu uliopita.
Mo Salah alifunga bao Jumapili katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England msimu huu ambapo aliwasaidia Liverpool kuwalaza West Ham 4-0.
Mabao hayo mengine yalifungwa na Sadio Mane (mawili) na Daniel Sturridge.
Mo Salah achunguzwa Mo Salah achunguzwa Reviewed by habari motto on 7:02 AM Rating: 5

Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda

6:57 AM
Image result for Robert Kyagulanyi
Mbunge nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu kama Boni Wine amekamatwa na polisi saa kadhaa baada ya dereva wake kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi.
Awali Bobi Wine alidai kuwa dereva wake aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya gari lake.
Mbunge huyo wa Kyadondo aliandika kwenye mtandao wa Twitter kuwa walikuwa eneo linalojulikana kama Arua kwenye kampeni wakati mauaji hayo yalitokea.
Uchaguzi mdogo unatarajiwa kuandaliwa eneo hilo siku ya Jumatatu katika juhudi za kumtafuta yule atakayechukua mahala pake mbunge aliyeuawa Ibrahim Abiriga .
Bobi Wine na viongozi kadhaa wa upinzani walikuwa eneo hilo kumuunga mkono mgombea huru Kassiano Wadri.
Mikutano hiyo ilienda sawa siku yote kabla ya polisi kuanza kukabiliana na wafuasi wa Wadri.
Wafuasi wa Wadri nao waliripotiwa kukabiliana na wale wa mgombea wa NRM Tiperu Nusura.
Bobi Wine pia aliandika kuwa hoteli yake ilizingirwa na polisi kufuatia visa hivyo.
Hata hivyo polisi wanasema kuwa wafuasi wa upinzani watalaumiwa kwa kuuliwa dereva huyo wa Bobi Wine Yasin Kawuma.
Msemaji wa polisi Emilian Kayima, anasema watu waliokuwa wamevaa shati za kampeni za mgombea Wadri, walianza kuurushia mawe msafara wa rais hali ambayo ilisababisha polisi kufyatua risasi.
"Mwendo wa saa kumi na mbili unusu jioni msafara wa rais ulishambuliwa na wahuni katika manispaa ya Arua wakati rais alikuwa anaondoka uwanja wa Boma ambapo alikuwa amefanya mkutano wa mwisho," Kayima alisema.
Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda Mbunge Bobi Wine akamatwa Uganda Reviewed by habari motto on 6:57 AM Rating: 5

Vipindi vya stesheni za Tanzania Kuonyeshwa Bure

6:55 AM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe
Image captionWaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwanyembe
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania ,Dr.Harrison Mwakyembe, amezitaka kampuni za vin'gamuzi vya DSTV, AZAM na ZUKU kufuata sheria kwa sababu Watanzania wana haki ya kupata habari bila kulipishwa.
Waziri huyo ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) izipe utaratibu kampuni hizo namna ambavyo zinaweza kurusha chaneli za ndani bure kama wamevutiwa na soko hilo.
Tanzania ilipoingia katika mfumo wa digitali kumekuwa na mfumo wa kulipia na hapo mwanzoni Tv zote zilikubaliana na zilipewa masharti kwa mfano mtazamaji anapata gharama mwanzoni tu anaponunua king'amuzi .
Wamiliki wa vin'gamuzi hivyo vya DSTV ,AZAM na ZUKU wote makao makuu yao yako nje ya nchi na maudhui yao ni ya kimataifa hivyo hata gharama za ulipaji wao leseni ni tofauti lakini ikija kwenye suala la matangazo ya ndani utaratibu upo pia na wanapaswa kuufuata.
"Kama hawa wenzetu wana hamu sana na soko hili la ndani waende TCRA wapewe utaratibu wa namna ya kuupata," amesema Mwakyembe.
Waziri Mwakyembe alisisitiza kuwa ni haki ya Mtanzania kuweza kuhabarishwa kwa sababu chanzo cha mapato sio watazamani bali ni matangazo ndio maana hizi chaneli za umma wanatakiwa walipwe na maudhuhi yake ni ya ndani ya nchi.
Kuna mfumo wa kulipia lakini TBC, Star TV, ITV, Channel Ten na EATV ni lazima zirushwe bila malipo yoyote .
Dk. Mwakyembe pia amesisitiza kuwa serikali haijafuta leseni za visimbuzi/Ving'amuzi vya Azam, Zuku na DSTV Multichoice Tanzania bali wanawataka kuondoa chaneli ambazo zinatakiwa kurushwa bure kulingana na matakwa ya mikataba yao.
Vipindi vya stesheni za Tanzania Kuonyeshwa Bure Vipindi vya stesheni za Tanzania Kuonyeshwa Bure Reviewed by habari motto on 6:55 AM Rating: 5

Hii ndiyo Miji bora zaidi kuishi duniani

6:51 AM

Couple in Vienna
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mji mkuu wa Austria, Vienna, umeorodheshwa kuwa mji bora zaidi kwa watu kuishi duniani, na kuchukua nafasi ya mji wa Melbourne wa Australia ambao umeongoza kwa miaka mingi.
Mji wa Harare, Zimbabwe ni miongoni mwa miji ambayo haivutii kwa watu kuishi duniani.
Ni mara ya kwanza kwa jiji la bara Ulaya kuongoza kwenye orodha hiyo ya kila mwaka ambayo huandaliwa na Kitengo cha Uchunguzi cha Jarida la Economist.
Utafiti huo uliorodhesha miji 140 duniani kwa kufuata vigezo mbalimbali vikiwemo uthabiti wa kisiasa na kijamii, visa vya uhalifu, elimu na kupatikana kwa huduma bora ya afya.
Katika utafiti huo, jiji la Manchester ndilo lililoimarika zaidi miongoni mwa miji ya Ulaya ambapo jiji hilo lilipanda hatua 16 hadi nafasi ya 35.
Jiji hilo limo mbele ya London kwa hatua 13, ambalo ndilo pengo kubwa zaidi kwa miji hiyo miwili kwenye orodha hiyo tangu kuanza kuandaliwa kwa orodha hiyo miongo miwili iliyopita.
Jarida la Economist limesema kuimarika kwa Manchester ni kwa sababu ya kuimarishwa kwa usalama.
'Ukakamavu'
Utafiti huo ulikosolewa mwaka jana kwa kuushusha hadhi mji wa Manchester baada ya shambulio la Manchester Arena ambapo watu 22 waliuawa.
Mwaka huu, mhariri wa utafiti huo Roxana Slavcheva amesema jiji la Manchester "limenyesha ukakamavu na kujikwamua kutoka kwa shambulio hilo la kigaidi ambalo lilikuwa imetikisa uthabiti wake.
Bi Slavcheva amesema usalama pia umeimarika katika miji kadha ya Ulaya magharibi.
Kuongoza kwa Vienna ni iashara ya kurejea kwa utulivu kiasi katika maeneo mengi ya Ulaya.
Melbourne ilikuwa awali imeongoza kwa miaka saba mtawaliaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMelbourne ilikuwa awali imeongoza kwa miaka saba mtawalia
Kwa mujibu wa utafiti huo, karibu nusu ya miji imeimarika katika mwaka mmoja uliopita.
Melbourne, ambao kwa sasa ni mji wa pili duniani kwenye orodha hiyo, ilikuwa imeongoza kwa miaka saba mfululizo.
Majiji mengine mawili ya Australia pia yamo kwenye orodha ya kumi bora mwaka huu: Sydney na Adelaide.
Upande ule mwingine, mji mkuu wa Syria, Damascus ambao umeathiriwa sana na vita ndio usiopendwa zaidi na watu duniani ukifuatwa na Dhaka nchini Bangladesh na Lagos nchini Nigeria.
Economist wanasema kwamba uhalifu, machafuko, ugaidi na vita vilichangia sana katika kuorodheshwa chini kwa miji iliyoshika mkia.
DamascusHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Miji bora zaidi kuishi duniani 2018
1. Vienna, Austria
2. Melbourne, Australia
3. Osaka, Japan
4. Calgary, Canada
5. Sydney, Australia
6. Vancouver, Canada
7. Tokyo, Japan
8. Toronto, Canada
9. Copenhagen, Denmark
10. Adelaide, Australia

Hii ndiyo Miji bora zaidi kuishi duniani Hii ndiyo Miji bora zaidi kuishi duniani Reviewed by habari motto on 6:51 AM Rating: 5

SERIKALI KUDHIBITI UHALIFU UKANDA WA ZIWA NA BAHARI

6:19 AM
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akiwaongoza viongozi wengine kutembelea eneo la mwambao wa Ziwa Victoria baada ya kuikabidhi boti hiyo ya doria kwa Jeshi la Polisi, kutoka kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Daniel Shilla, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel na Diwani wa Chato, Richard Bagolele. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Daniel Shilla akimshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kumkabidhi Kituo cha Polisi kinachohamishika wilayani Chato.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyeshika koti), akishuka katika boti maalumu aliyowakabidhi Kikosi cha Polisi wilayani Chato ikiwa ni mkakati wa Serikali kupambana na uhalifu katika ukanda wa Ziwa na Bahari nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel, akishuka katika boti maalumu iliyokabidhiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani) kwa Kikosi cha Polisi Wanamaji wilayani Chato, ikiwa ni mkakati wa Serikali kupambana na uhalifu katika ukanda wa Ziwa na Bahari nchini.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.



Na Mwandishi Wetu

Serikali imejipanga kuimarisha Ulinzi na Usalama katika Ukanda wa Ziwa na Bahari kote nchini ili kuweza kudhibiti uhalifu unaotekelezwa majini ikiwepo uvuvi haramu, usafirishaji wa magendo na uhalifu mwingine unaotokea katika maeneo ya ziwa na bahari.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya boti maalumu ya doria na ufunguzi wa Kituo cha Polisi Wanamaji, wilayani Chato, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha inadhibiti uhalifu katika Ukanda wa Ziwa na Bahari kwa kutumia Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya serikali, ili kuhakikisha wananchi wanafanya shughuli za kuchumi bila ya kuwa na wasiwasi juu ya usalama wao 

Alisema moja ya changamoto kubwa aliyoelezwa wakati alivyofanya ziara ya awali wilayani Chato ni kuwepo kwa matukio ya uhalifu ziwani yaliyopelekea baadhi ya wananchi kusitisha shughuli za kiuchumi katika mwambao huo wa Ziwa Victoria.

“Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuleta maendeleo katika nyanja zote na kuwawekea mazingira mazuri wananchi wake kujishughulisha na shughuli za kiuchumi, hivyo basi tutahakikisha tunaimarisha ulinzi katika sehemu zote ambazo wananchi wanafanya shughuli zao ikiwepo ukanda wa ziwa na bahari na leo hii tunaanzia hapa wilayani Chato.

“Pia nawasihi askari polisi kufanya kazi kwa maadili na agizo hili nalitoa kwa nchi nzima na serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi aitomvumilia askari yoyote atakaebainika kuwabambikia kesi wananchi,hatua kali zitachukuliwa kwa atakaebainika” alisema Masauni ambae pia ni Mbunge wa Kikwajuni

Naye Diwani wa Kata ya Muungano, wilayani Chato,Johnson Kilimokwanza alisema anaishukuru serikali kwa kuleta boti hiyo na ufunguzi wa kituo cha polisi kwani moja ya changamoto iliyokuwa inawasumbua wavuvi katika mwambao huo ni masuala ya uhalifu unaotokea ziwani huku akiweka wazi uwepo wa kituo na boti ya doria vitapunguza masuala ya uhalifu.

Mmoja wa askari polisi ambae hakupenda jina lake litajwe alisema wao wanaishukuru serikali kwa kuwaletea boti na kituo ambavyo vitawarahisishia kupambana na uhalifu 


“Muhimu naomba serikali pia waweze kutuletea gari ambalo litasaidia pia katika mapambano hayo ya uhalifu kama unavyoona tayari tuna kituo hapa cha wanamaji naibu waziri amekizindua,muhimu sasa tuletewe usafiri utakaowezesha kupeleka mahabusu mahakamani,” alisema askari polisi huyo.
SERIKALI KUDHIBITI UHALIFU UKANDA WA ZIWA NA BAHARI SERIKALI KUDHIBITI UHALIFU UKANDA WA ZIWA NA BAHARI Reviewed by habari motto on 6:19 AM Rating: 5

Waziri Mwakyembe aitaka TCRA kutoa muongozo kwa wenye visimbuzi nchini

6:15 AM
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe  ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) kufanya mazungumzo na wamiliki wa visimbuzi vya AZAM, DSTV na ZUKU ili kutoa muongozo wa nini kifanyike juu ya hatma yao ya kutoruhusiwa kuonesha channeli za umma kinyume leseni zao.
 
Akizungumza hayo na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Waziri Mwakyembe alisema kuwa visimbuzi vya AZAM, DSTV na ZUKU vilikiuka mkataba wao wa leseni na kuonesha chaneli za umma ikiwa ni pamoja na kuwatoza fedha watazamaji.
 
“TCRA watoe muongozo wa nini kifanyike kwa visimbuzi vilivyokiuka utaratibu, ikiwa sasa watapenda kuonesha channeli hizo za umma wapewe utaratibu wa nini cha kufanya” alisema Waziri Mwakyembe
 
Aliongeza kuwa uamuzi wa TCRA kuwataka watoe channeli hizo za umma umezingatia sheria, ambapo amevipongeza visumbuzi hivyo kwa kufuata sheria na kutoendelea kuonesha channeli hizo.Aidha, Waziri Mwakyembe alifafanua kuwa visimbuzi vinavyoruhusiwa kuonesha channeli za umma bila kuwatoza fedha watazamaji ni Startimes, Digtek na Continental, kulingana masharti ya aina ya leseni yao.
 
Alitaja masharti hayo kuwa ni visimbuzi hivyo vimelipa gharama ya leseni mahsusi ambayo ni dola laki nne, miundombinu ya urushaji matangazo yake iko hapa nchini ambayo ni minara na satellite, maudhui yake ni yakitanzania na gharama ya visimbuzi vyao ni nafuu.
 
Waziri Mwakyembe, alisema kuwa masharti ya leseni ya kurusha maudhui ama channeli za kulipia ni pamoja na gharama ndogo ya leseni ambayo ni dola laki moja, maudhui yake ni kwa ajili ya soko la kimataifa.
 
Aliongeza masharti mengine kuwa ni, miundombinu ya kurusha matangazo ipo nje ya nchi mfano ya DSTV iko Dubai, ZUKU nchini Kenya na AZAM ikiwa  huko nchini Mauritius, pamoja na matangazo yake kutegemea kurushwa kwa satelite.
 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa ufafanuzi juu ya visimbuzi visivyoonesha chaneli za ndani mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Afisa Mwandamizi Mkuu wa Sheria toka Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Dk. Philip Filikunjombe na kulia ni Afisa Mwandamizi Mkuu wa Masuala ya Utangazaji toka mamlaka hiyo Bw. Andrew Kisaka.
Waziri Mwakyembe aitaka TCRA kutoa muongozo kwa wenye visimbuzi nchini Waziri Mwakyembe aitaka TCRA kutoa muongozo kwa wenye visimbuzi nchini Reviewed by habari motto on 6:15 AM Rating: 5

Dk Bashiru Ali ateuliwa Katibu Mkuu mpya wa CCM

10:45 PM
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) alipokuwa akizungumza na kumpongeza Dk.Bashiru Ali (kulia) mara baada ya kuteuliwa na kupata ridhaa ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC)kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(katikati),[Picha na Ikulu.] 29/05/2018.
 Katibu Mpya wa CCM Taifa Dk.Bashiru Ali (kulia) mara baada ya kuteuliwa na kupata ridhaa ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 29/05/2018.
 Katibu Mpya wa CCM Taifa Dk.Bashiru Ali (kulia) alipokuwa akiwashukuru Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) mara baada ya kuteuliwa na kupata ridhaa ya   kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  katika Mkutano ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Nd,Rodrik Mpogolo [Picha na Ikulu.] 29/05/2018.
 Wajumbe wa Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) wakinyanyua mikono juu kuashiria kuunga mkono uteuzi wa Katibu Mpya wa CCM Taifa Dk.Bashiru Ali wakati wa Mkutano ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(hayupo pichani),[Picha na Ikulu.] 29/05/2018.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) alipokuwa akimpongeza Dk.Bashiru Ali (kulia) mara baada ya kuteuliwa na kupata ridhaa ya Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli(katikati),[Picha na Ikulu.] 29/05/2018.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein(kushoto) alipokuwa akimuonesha kitu  Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli wakati wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa  ulioendelea leo katika Ukumbi wa   Kiwete Ikulu Jijini Dar es Salaam,[Picha na Ikulu.] 29/05/2018.
Dk Bashiru Ali ateuliwa Katibu Mkuu mpya wa CCM Dk Bashiru Ali ateuliwa Katibu Mkuu mpya wa CCM Reviewed by habari motto on 10:45 PM Rating: 5

Albert Msando Kuongoza Kamati Ya Makonda Kusaka Haki za Watoto

6:33 AM
Albert Msando Kuongoza Kamati ya Makonda ya Kutafuta Haki ya Watoto
Wakili Albert Msando ataongoza kamati iliyounda na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda kwa ajili ya kushughulikia kesi zote na changamoto zilizojitokeza katika zoezi la kutafuta haki za watoto waliotelekezwa na wazazi wao.
Zoezi hilo lilifungwa hapo jana April 27, 2018 ambapo wananchi 17,000 walijitokeza, kati yao 7,184 walisikilizwa, huku 270 wakipimwa DNA.
RC Makonda ameunda Kamati ya Wataalamu 15 wakiwemo Wanasheria, Maafisa Ustawi wa Jamii, Jeshi la Polisi Dawati la jinsia na Asasi za kiraia itakayofanya kazi ya kupitia mapungufu ya kisheria na Changamoto zilizojitokeza.
Kamati hiyo ambayo itaanza kazi rasmi May 05, 2018 chini ya Wakili Albert Msando ambaye ndiye Mwenyekiti wake itatoa mapendekezo kwaajili ya kufikishwa kwa mamlaka husika ili kufanyiwa maboresho.
Utakumbuka December 20, 2017 Wakili Albert Msando aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli katika tume itakayokuwa na jukumu la kufuatilia mali za Chama cha Mapinduzi (CCM).
Kabla ya kuteuliwa na Rais Magufuli, September 26, 2017 Wakili Msando aliteuliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrion Mwakyembe kuwa Mjumbe wa kamati ya kupitia sheria ya Hakimiliki za kazi za wasanii.
Albert Msando Kuongoza Kamati Ya Makonda Kusaka Haki za Watoto Albert Msando Kuongoza Kamati Ya Makonda Kusaka Haki za Watoto Reviewed by habari motto on 6:33 AM Rating: 5

Kamishna wa zamani wa mji wa Dar es Salaam aaga dunia

6:22 AM
Image result for Abbas Kandoro
Aliyekuwa kamishna wa eneo la Mbeya na mji wa Dar es Salaam Abbas Kandoro ameaga dunia katika hospitali kuu ya Muhimbili (MNH).
Habari hizo zilithibitishwa na msemaji wa hospitali hiyo Aminiel Aligaesha.
Bwana Kandoro alifariki siku ya Ijumaa, Aprili 27, 2018 wakati alipokuwa akipata matibabu.
Alifariki katika hospitali hiyo siku hiyohiyo aliyolazwa.
Kulingana na familia yake maombi ya mwisho ya marehemu yatafanyika katika msikiti wa Manyema uliopo Kariakoo mjini Dar es Salaam ambapo waombolezaji watakuwa na fursa ya mwisho kuuaga mwili.
Mwili wake baadaye utasafirishwa hadi mjini Iringa kwa mazishi kulingana na ripoti za gazeti la The Citizen Tanzania.
Image result for Abbas Kandoro
Rais John Pombe Magufuli alituma salamu za rambirambi kwa familia ya Kandoro . Raisi Magufuli amesema kuwa ameshangazwa na kifo cha marehemu, akisema kuwa mchango wake katika kubadili sekta ya huduma za umma utakumbukwa.
Kabla ya kifo chake, marehemu alikuwa amehudumu katika afisa tofauti za umma kama kamishna na mkuu wa wilaya ya Tabora , Arusha , mwanza na Mbeya 
NA BBC
Kamishna wa zamani wa mji wa Dar es Salaam aaga dunia Kamishna wa zamani wa mji wa Dar es Salaam aaga dunia Reviewed by habari motto on 6:22 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.