STAA WA BONGO MOVIE APATA AJALI

Taswira baada ya ajali hiyo.
 STAA wa filamu za Kibongo, anayepatia zaidi kuigiza kama Mchungaji, Emmanuel Myamba ‘Pastor Myamba’ amepata ajali baada ya gari lake aina ya Toyota Creasta kugongwa na gari lingine jana  mchana katikati ya Boko na Bunju jijini Dar es Salaam.
 Katika ajali hiyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa zaidi ya magari hayo mawili kuharibika. 

Kwa mujibu wa Pastor Myamba, dereva aliyekuwa akiendesha gari lililogonga gari lake alitokomea na kuacha gari lake eneo la tukio baada ya kugundua kuwa ndiye aliyekuwa na makosa. 
Magari yote mawili yamevutwa na 'breakdown' kisha kupelekwa kituo cha polisi Tegeta.
STAA WA BONGO MOVIE APATA AJALI STAA WA BONGO MOVIE APATA AJALI Reviewed by habari motto on 10:46 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.