Baadhi ya silaha zilizokamatwa na jeshi la polisi.
Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza Kova.
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia mtu mmoja anayefahamika kwa jina
la Gunner Meena (40) mkazi wa Kinyerezi, Segerea, Dar es Salaam, kwa
tuhuma za kujifanya mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa .
Tukio la mwisho lililomfanya akamatwe ni pale alipomtishia mfanyabiashara
mwenye asili ya Kisomali aitwaye Abdi Dalmar, ili ampe Tshs
25,000,000/= ama sivyo angechukua hatua chini ya Sheria ya Usalama wa
Taifa.
Aidha jeshi hilo
katika kuendesha oparesheni zake za kutokomeza ujambazi wa kutumia
silaha limefanikiwa kukamata bastola nne na shot-gun moja wiki hii.
AFISA USALAMA FEKI AKAMTWA,SHUHUDIA SILAHA ZAKE HAPA
Reviewed by habari motto
on
9:17 PM
Rating: