AJALI MBAYA YATOKEA, WATU ZAIDI YA 40 WAPOTEZA UHAI


Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS lenye nambari za usajili T 677 CYC lililokuwa likitoka 
Musoma kuelekea Silari Mkoani Mara likiwa limeumia vibaya sana baada ya kugongana 
uso kwa uso na Basi lingine la Kampuni ya MWANZA COACH lenye nambari za usajili 
T 736 AWJ katika eneo la SabaSaba,Mjini Musoma mchana huu.Watu zaidi ya 35 
wamepoteza maisha papo hapo na wengika kujeruhiwa vibaya sana.kwa mujibu wa 
Ripota wetu aliopo eneo la tukio hivi sasa,inaelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo Basi la J4
 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili
 T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa 
wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi liliweza kuisukuma 
kwa ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka
 kwenye njia na kwenda kuingia mtoni.hali iliyoipelekea basi hiyo kuamini kuwa itawahi 
kupita katika daraja hilo bila kufahamu kuwa Basi lingine linalokuja mbele nalo liko 
kwenye mwendo kasi huku nalo likitaka kuwahi kupita kwenye daraja hilo.Ndani ya gari
 hiyo ndoho kulikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki na mmoja amejeruhiwa.
Picha na Ahmad Michuzi,Musoma.
Basi la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS. 


Umati wa Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya na 
kusababisha watu 25 kupoteza maisha pamoja hapo.wakishuhudia tukio hilo la ajali. 


Guldoza likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za 
usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka kuingia mtoni.Gari hii ilikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa. 


Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo. 

Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio. 


Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha. 

Uokozi ukiendelea. 

Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo. 


 KWA HABARI ZAIDI YA TUKIO HILI BOFYA HAPA

AJALI MBAYA YATOKEA, WATU ZAIDI YA 40 WAPOTEZA UHAI AJALI MBAYA YATOKEA, WATU ZAIDI YA 40 WAPOTEZA UHAI Reviewed by habari motto on 10:15 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.