AMWAGA RAZZI ONYESHO LA SIKINDE

Binti akivamia jukwaa baada ya kupiga urabu wa kutosha.
BINTI mmoja aliyeonekana kuzidisha kiburudisho, mwishoni mwa wiki iliyopita alitibua onyesho na kugeuka kuwa burudani baada ya kupanda juu ya jukwaa la Mlimani Park ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’ na kuwakumbatia ovyo wanamuziki.

Tukio hilo lilitokea wiki iliyopita katika ukumbi wa Railway Club ambako paparazi wetu alimshuhudia binti huyo aliyefahamika kwa jina moja la Fatma, akianza kubadilika taratibu kadiri alivyokuwa akipata kiburudisho chake kilichokuwa katika vipakti vya plastiki.


Akizidi kusumbua jukwaa.
Licha ya kuwakumbatia, pia msichana huyo alivuruga shoo hiyo baada ya kukanyaga nyaya zinazounganisha vyombo vya muziki vya bendi hiyo na kusababisha umeme kuzimika jukwaani, hivyo kusababisha onyesho kusimama kabla ya mafundi mitambo kurekebisha hitilafu.
AMWAGA RAZZI ONYESHO LA SIKINDE AMWAGA RAZZI ONYESHO LA SIKINDE Reviewed by habari motto on 8:57 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.