Auawa baada ya kushidwa kujieleza


MTU mmoja mwenye umri kati ya miaka 25 na 30 ambaye jina
lake halifahamiki, ameuawa baada ya kushindwa kujieleza juu
ya pikipiki ambayo yeye na mwenzake walikuwa wanajaribu
kuiuza Chalinze
Watu hao walifika Chalinze wakidai kutokea Gairo wakitaka
kuuza pikipiki aina ya Toyo yenye namba za usajili T 336 BZC.
Lakini walipobanwa kuhusu kadi ya pikipiki walibabaika na hivyo
kuanza kupigwa ambapo mmoja alitoroka na huyo mwingine
kuuawa kwa kuchomwa moto baada ya kipigo.
Tukio hilo limethibitishwa na kaimu kamanda wa Polisi Mkoa wa
Pwani, Athuman Mwambalaswa.
Kamanda huyo alisema kwamba tukio hilo lilitokea Septemba 25
mwaka huu, majira ya saa 1 asubuhi eneo la Pera Chalinze
wilaya ya Bagamoyo.
Kamanda huyo aliwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria
mkononi kwani ni kinyume cha sheria na kuwataka kuwapeleka
kwenye vyombo vya sheria, ikiwa ni pamoja na polisi ili hatua
stahiki ziweze kuchukuliwa.
Auawa baada ya kushidwa kujieleza Auawa baada ya kushidwa kujieleza Reviewed by habari motto on 11:58 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.