KUTOKA KWA KASSIM MGANGA KUHUSU VIDEO YAKE MPYA.. "YA MOTTO"

Tajiri wa Mahaba Cassim Mganga mwezi June 2014 aliachia wimbo mpya unaoitwa ‘Moto moto’. Wimbo huo ulikuwa tayari umefanyiwa video toka mwaka jana (2013) lakini kulikuwa na taarifa za mtaani zilizodai kuwa video hiyo iliyomgharimu pesa nyingi iliharibika ndio maana haijatoka hadi leo ikiwa ni zaidi ya mwaka.
cassim
Mganga amekanusha taarifa hizo na kusema video hiyo haijaharibika isipokuwa inahitaji marekebisho kidogo na itatoka.
“video ya moto moto inakuja, moto ni vitu vidogo tu vya kuviswitch kidogo tu, ingawa tunahitaji kuongeza baadhi ya clip basi, hakuna video kufutwa hakuna video hatuitaki hakuna nini. Ukioneshwa video hapa utatamani video itoke, kila mtu ninayemuonesha ebana hiyo video noma video kali kwanini isitoke, lakini sisi na jicho letu la tatu unajua, unaefanya siku zote ndiye unaona”. Cassim aliiambia 255 ya XXL.
KUTOKA KWA KASSIM MGANGA KUHUSU VIDEO YAKE MPYA.. "YA MOTTO" KUTOKA KWA KASSIM MGANGA KUHUSU VIDEO YAKE MPYA.. "YA MOTTO" Reviewed by habari motto on 11:59 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.