MSANII SANDRA AONYESHA UTOFAUTI NA WASANII WENGINE WENGI BONGO MOVIE


MSANII wa siku nyingi katika tansia ya filamu Bongo, Salama Salmin ‘Sandra’ amefunguka kuwa tangu ameanza kujihusisha na mambo ya sanaa hajawahi kuwa na bwana ndani ya klabu ya Bongo Movies na wala hajawahi kutoa rushwa ya ngono kwa ‘dairekta’ kama ilivyo kwa wengine.

Akizungumza na paparazi hivi karibuni, Sandra alisema kuna baadhi ya wasanii wanafikiri kuwa na mwanaume ndani ya Klabu ya Bongo Movie ndiyo kutimiza ndoto zao kumbe ni kujidharaulisha tu.
 

“Sina bwana wala sijawahi kutoa rushwa ya ngono kwa ‘dairekta’ na sifikirii kufanya hivyo kamwe, maana ni kujishushia heshima yangu  wakati mimi ni mke wa mtu na wala siwezi  kunadi mwili wangu,” alisema Sandra
MSANII SANDRA AONYESHA UTOFAUTI NA WASANII WENGINE WENGI BONGO MOVIE MSANII SANDRA AONYESHA UTOFAUTI NA WASANII WENGINE WENGI BONGO MOVIE Reviewed by habari motto on 8:03 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.