NA HIKI NDICHO ALICHOKISEMA CHRISTIAN RONALDO BAADA YA MAN U KUMSAJILI FALCAO

Cristiano Ronaldo (7)
MSHAMBULIAJI Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameupongeza usajili wa Radamel Falcao (pichani juu) kwenda Manchester United na kusema na manunuzi bab kubwa kwa Van Gaal.
Usajili huo wa mkopo wa wa mwaka mmoja, utaigharimu Manchester United pauni milioni 12 na hivyo kufikia matumizi ya pauni milioni160 katika usajili wa kiangazi hiki baada ya kuwanasa pia Angel di Maria, Daley Blind, Luke Shaw, Ander Herrera na Marcos Rojo.
“Nadhani ni manunuzi sahihi. Manchester United haijaanza vizuri, pointi mbili hadi hivi sasa, hivyo wanahitaji wachezaji wa hali ya juu na Falcao ni mchezaji wa hali ya juu,” alisema Ronaldo nyota wa zamani wa Manchester United.
Mshambuliji wa zamani wa Liverpool, Michael Owen ambaye aliwahi kuichezea United, nae pia amepongeza usajili huo lakini akawa anajiuliza ni vipi kikosi cha timu hiyo kitapangika.
“Pengine United inaweza kuwatumia washambuliaji wote watatu kwa pamoja (Rooney, Falcao na Van Persie), ikiwa hivyo basi Juan Mata atakuwa hatarini kusota benchi,” alisema Owen na kuongeza: “Nadhani mbuzi wa sadaka atakuwa Juan Mata”
NA HIKI NDICHO ALICHOKISEMA CHRISTIAN RONALDO BAADA YA MAN U KUMSAJILI FALCAO NA HIKI  NDICHO ALICHOKISEMA CHRISTIAN RONALDO BAADA YA MAN U KUMSAJILI FALCAO Reviewed by habari motto on 1:54 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.