UZINDUZI WA KIVUKO CHA KIGAMBONI

 Kivuko cha Mv Kigamboni kinavyoonekana kwa ndani, kinatarajiwa kuanza kutumika siku ya alhamisi baada ya matengenezo yalifanywa na Jeshi la Wanamaji  kwa mda wa wiki tatu tangu kilipoaacha kufanya kazi Agosti 14 mwaka huu.
 Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli  akiongea na wajumbe mbalimbali waliofika katika  uzinduzi wa kivuko cha kigamboni  leo jijini Dar es  Salaam kinachofanyiwa matenganezo  na Jeshi la Wanamaji maeneo ya kurasini ,ambacho kinatarajiwa kuanza kutumika rasmi alhamisi wiki hii.
 Mtendaji  Mkuu  Temesa Injinia  Marceline Magesa akitoa neno la shukrani  kwa Jeshi la Wanamaji waliwezesha matengenezo ya Mv Kigamboni  leo jijini Dar es Salaam ambapo kinatarajiwa kuanza kutumiwa na wananchi wiki hii.
 Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli ( kushoto) na Katibu Mkuu wa Ujenzi  Injinia Mussa Iyombe(kulia) wakisikiliza kwa makini maelekezo yaliyokuwa yakitolewa katika ufunguzi wa kivuko cha Mv Kigamboni leo jijini Dar es Salaam kinachofanyiwa matenganezo  na Jeshi la Wanamaji maeneo ya kurasini  na kinatarajiwa kuanza kutumika wiki hii.
 Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli ( katikati mwenye suti nyeusi) akielekea katika eneo  ambalo kivuko cha MV Kigamboni  kilipo kwa ajili ya ukaguzi wa kazi iliyofanywa na wahandisi wa Jeshi la Wanamaji leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli ( katikati) akipata maelekezo kutoka kwa  Msimamizi wa matengenezo  Luten Kanali Abel Gwanafyo (Kulia), kushoto  ni  Mkuu wa Jeshi la Maji Brigadia Jenerali Rostian Laswai wakati wa ufunguzi wa kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam ,amabapo  kinatarajiwa kuanza kutumika wiki  kurahisisha usafiri kwa watu wa  Kigamboni.
 Waziri wa Ujenzi  Dkt. John Magufuli ( katikati) akipata maelekezo kutoka kwa  Msimamizi wa matengenezo  Luten Kanali Abel Gwanafyo (Kulia), kushoto  ni  Mkuu wa Jeshi la Maji Brigadia Jenerali Rostian Laswai wakati wa ufunguzi wa kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam ,amabapo  kinatarajiwa kuanza kutumika wiki  kurahisisha usafiri kwa watu wa  Kigamboni.

Kivuko cha Mv Kigamboni kinavyoonekana  upande wa mbele na ubavuni , kikiwa katika hatua za mwisho tayari kwa kuanza  kutumiwa na wananchi siku ya alhamisi baada ya matengenezo yaliofanywa na Jeshi la Wanamaji  kwa mda wa wiki tatu tangu kilipoaacha kufanya kazi Agosti 14 mwaka huu. Picha na Lorietha Laurenc eMaelezo
UZINDUZI WA KIVUKO CHA KIGAMBONI UZINDUZI WA KIVUKO CHA KIGAMBONI Reviewed by habari motto on 12:41 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.