Habari zilizotufikia hivi punde kutoka mjini Kahama ni kwamba Basi la Wibonela likitoka Kahama kwenda jijini Dar es salaam limepata ajali asubuhi hii katika eneo la Phantom.
Mwandishi wa Malunde1 blog Ndalike Sonda kutoka Kahama anasema ajali hiyo imetokea asubuhi hii baada ya basi kumshinda dereva katika kona ya Phantom na kusababisha aruke kutoka kwenye basi hilo la kufanya basi hilo liviringike mara kadhaa.
Habari zinasema kuwa watu zaidi ya watano wamefariki dunia,na wengine kadhaa kujeruhiwa na wanakimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa ajili ya matibabu.
NA Malunde1 blog |