KINANA AMWAGA SIFA TELE KWA MEMBE NA NAPE KWA UCHAPAKAZI WAO

 
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikamua ng'ombe maziwa wanofugwa na watawa katika Kijiji cha Narunyu Kiwalala, Jimbo la Mtama, Lindi Vijijini, wakati wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi leo.  Kinana akizungumza na baadhi ya Watawa wa Kanisa Katoliki la Narunyu ambao wana mradi ng'ombe wa maziwa  Kinana akizungusha mashine ya kutenganisha ubora wa korosho katika kikundi hicho cha wananwake cha kubangua korosho katika Jimbo la Mtama ambalo Mbunge wake ni Bernard Membe.Kinana alimsifia kwa uchapakazi Mbunge wa Jimbo la Mtama, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Pia alimsifia Nape kwa utendaji wake ambapo alisema ana uwezo wa hali ya juu.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG  Kinana akisaidia kubangua korosho katika kikundi hicho cha Wanawake cha kubangua korosho  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia mbele ya Jengo la Mbunge wa Jimbo hilo, Bernard Membe ambaye amelijenga katika Kijiji cha Mtama, Lindi Vijijini  Wazee wa mji wa Mtama wakishangilia wakati Nape Nnauye akihutubia katika Makao Makuu ya Jimbo la Mtama  Kinana akisalimiana na Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Mtama, Masoud Ali Chitende wakati wa mkutano huo  Kinana na Membe wakishikana mikono na makatibu wa CCM wa matawi ikiwa ni ishara ya kuwakabidhi baiskeli zilizonunuliwa na Nape Nnauye na Membe  Kinana aakikabidhi bati 20 zilizonunuliwa na Nape Nnauyena Mbunge kwa ajili kuezekea Jengo la Kituo cha Polisi cha Mtama  Wananchi wakiwa wameuzuia msafara wa Kinana katika eneo la Nyangamara Jimbo la Mtama, wakitaka Kinana awasaidie ujenzi wa Ofisi ya Tawi la CCM.  Mbunge wa Jimbo la Mtama, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (katikati) akielezea mbele ya wananchi jinsi anavyokerwa na tabia ya baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Lindi kuliteka gari la wagonjwa la Kata ya Nyamangara. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na Nape Nnauye  Mkuu wa Mkoa wa Lindi Magarula S Magarula akitoa amri katika mkutano huo gari hilo lililotekwa na Uongozi wa Wilaya ya Lindi Vijijini  Wananchi wakishangilia kwa furaha baada ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Magarula S Magarula kuamuru gari la wagonjwa lirudi katika Kata hiyo  Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akishangiliwa baada ya kuwaambia kuwa ujenzi wa Zahanati ya Litipu utakamilika haraka  Kinana akisaidia ujenzi wa Zahanati ya Litipu ambayo kwa asilimia kubwa umegharamiwa na Membe  Membe akielezea kuhusu mradi wa maji  katika Kata ya Nyamangara Jimbo la Mtama  Kinana akihutubia katika alipokagua mradi wa maji katika Kata ya Nyamangara  Kinana akisaidia kuchimba mtaro katika Mradi wa Maji katika Kata ya Nyamangara, Mtama  Kinana akiagua Mradi wa Maji katika Kata ya Nyamangara  Kinana akiwasalimia wananchi alipowasili katika Kijiji cha Chiuta, Jimbo la Mtama  Nape Nnauye akishangiliwa na wananchi katika Kijiji cha Chiuta wakati wa mkutano wa hadhara  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, akicheza katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Chiuta  Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Chiuta  Kinana akigawa baiskeli kwa ajili ya kazi za Matawi ya CCM katika Kijiji cha Chiuta  Kinana akiwa na baadhi ya wanachama wapya wakati wa kuapa Kinana akizungumza baada ya kukagua Zahanati ya Chiuta
KINANA AMWAGA SIFA TELE KWA MEMBE NA NAPE KWA UCHAPAKAZI WAO  KINANA AMWAGA SIFA TELE KWA MEMBE NA NAPE KWA UCHAPAKAZI WAO Reviewed by habari motto on 9:45 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.