| Bw Rehani Athuman akiwasilisha mada leo New Dodoma hotel |
Mfuko wa taifa wa Huduma za Afya (NHIF) wameshauri Serikali kufikiria kuwa na Mamlaka ya Udhibiti wa gharama za matibabu nchini .
Hali hiyo imetokana na kuzidi kupanda kwa gharama za matibabu hasa dawa.
Kauli hiyo imetolewa na Mfuko huo kupitia Mkurugenzi wa CHF, Rehan Athuman wakati akiwasilisha mada kuhusu mwenendo wa mfuko huo kwa wanahabari mjini Dodfoma leo.
Alisema kumekuwepo na ufanisi mkubwa kwa mamlaka zilizoundwa za kudhibiti kupanda kwa bei ya mafuta na pia usafiri kulikotokana na kuwepo kwa EWURA na Sumatra.
Hata hivyo imeelezwa pia kwamba shauri hilo kwa sasa linafanyiwa kazi na Wizara ambayo kimsingi imekubali mapendekezo ya kuwa na utaratibu wa kudhibiti gharama za huduma za matibabu na kazi.
Imeelezwa kuwa kazi hiyo imeanza kwa utafiti wa gharama za matibabu nchini katika vituo vya matibabu.
Akizungumzia maendeleo ya mfuko alisema Bw. Rehani Athumani, alisema Mfuko utaendelea kuhamasisha na kusimamia matumizi sahihi ya fedha za uchangiaji ili fedha hizo ziboreshe upatikanaji wa dawa na huduma nyingine za matibabu.
Mfuko unawashauri Wakurugenzi wa Halmashauri nao wasimamie mwongozo wa Serikali matumizi ya fedha hizo.
Hiyo inatokana na ukweli kuwa kuna matumizi yasiyo sahihi katika masuala ya dawa hasa ukizingatia kwamba jumla ya Tzs 363.79 bn/= zimelipwa kwa watoa huduma wote waliosajiliwa (serikali, asasi za dini na za kujitolea na vituo vya binafsi) lakini vituo vya serikali bado vinakosa dawa kwa kubaki wakitegemea Bohari Kuu ya Madawa.
Akizungumzia uboreshaji wa huduma za maabara na uchunguzi alisema NHIF imetenga kiasi cha Tsh Bilioni 10 kwa mwaka 2013/14 ambapo zilizoidhinishwa ni Bilioni 5 na zilizotolewa ni Bilioni 2.098.
NHIF yaomba udhibiti gharama za matibabu
Reviewed by habari motto
on
11:20 AM
Rating: