MWANAMUZIKI Desire Luzinda anatafutwa na polisi baada ya Waziri wa Nchi wa Uganda anayeshughulikia maadili na heshima,Simon Lokodo kuagiza akamatwe ahojiwe kuhusu picha zake za utupu zilizochapishwa katika mitandao ya kijamii.
Mwanamuziki huyo, mama wa mtoto mmoja alishawahi kuomba radhi kwa picha hizo na kumshutumu mtalaka wake kwa kumfanyia visa baada ya kumwagana.
Mtalaka huyo amezimwaga picha hizo ambazo nyingine zimetumika katika magazeti akitaka kumfunza adabu.
Waziri huyo amewataka polisi kumkamata mwanamuziki huyo ili ajieleze imekuaje analeta shida katika mitandao ya jamii na kuvunja maadili.Luzinda, 26, ambaye tangu picha hizo kuchapishwa amejificha ana binti mdogo anayeitwa, Michelle Heather.
“Nilitopea katika mahaba,” anasema Luzinda “Sijawahi kupiga picha za utupu.mama yangu aliponipigia simu aliniuliza kama nilileweshwa kufanya vile, kwani aliamini si mimi na akili zangu, sikumjibu.”
Tayari Luzinda ameposti kumradhi katika vyombo vya habari vya kijamii na kuzungumza mambo sita
- Picha zangu ziliwekwa na mtu tyukliyeachana
- Kila mtu anakuwa na muda wa mahaba niue, lakini jamaa ameondoa imani yangu kwake,
- Najisikia vibaya kwa kupoteza akili yangu na kupiga picha zile za utupu za aibu,
- Mimi ni mtu msafi, mama wa mtoto mmoja na mwanamke mjasirimali
- Mamlaka zinafanya kila linalowezekana kuhakikisha nipata heshima yangu tena,
- Tafadhalini pokeeni kumradhi yangu.
"Kwa mashabiki wangu duniani kote, kumekuwa na maneno mengi katika vyombo vya jamii na habari kuhusu picha nilizopiga kwa siri ambazo zimefichuliwa na mpenzi tuliyeachana."
“Ukweli ni kuwa picha hizo zilichukuliwa faragha na mtu niliyempenda.Kuna dakika katika maisha yetu kila mtu anakuwa na kimuhemuhe chake. Lakini kiukweli nilimuamini mtu huyu, sikufikiria kitu kilichofanywa faragha kitatolewa hadharani hata kama tumehitilafiana.”
Nataka kuwaomba radhi mama yangu, mtoto wangu, familia yangu, marafiki zangu, mashabiki wangu na kila mtu ambaye ameguswa na tatizo hili. Kama nilivyosema picha hizi ni matokeo ya kuvunjwa kwa imani niliyokuwa nayo kwa mpendwa. Nawajibika kwa kupoteza akili na kupiga plicha hizo za aibu>Mtu huyo sit u kwamba amechezea imani yangu kwake lakini naona sasa anataka kushuudia anguko langu.
Mimi ni mtu safi, ni mama na mjariamali, picha hizi kw anamna yoyote zile haziniwakilishi mimi nilivyo. Kwa mashabiki wangu nawashukuru sana kwa kuwa name na kunitaka niwe mvumilivu. Nawashukuru sana
Picha za Utupu za Mwanamuziki Desire Wa Uganda Zamuingiza Matatani
Reviewed by habari motto
on
8:01 AM
Rating:
Reviewed by habari motto
on
8:01 AM
Rating:


