Breaking News: Wagombea Wajiondoa Kwenye Kinyanganyiro Baada Ya Kutishiwa Maisha,Kuchomewa Nyumba Zao, Simiyu


Wakati zoezi la kupiga kura uchaguzi wa viongozi wa serikali za mitaa kwa ngazi za vijiji, vitongoji pamoja na mitaa ukiendelea leo nchi nzima hali si shwari mkoani simiyu katika wilaya ya Busega.
  
Taarifa zilizotolewa na jeshi polisi Mkoani Simiyu pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo Paul Mzindakaya zinaeleza kuwa katika mji wa lamadi viongozi walikuwa wanagombea katika uchaguzi huo kupitia CCM wamejiondoa katika dakika za mwisho.

Taarifa hizo zilieleza kuwa viongozi hao wamejiondoa kwa madai ya kutishiwa kuuawa, kuchomwa moto nyumba zao ikiwa pamoja na familia zao kuuawa na wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
Breaking News: Wagombea Wajiondoa Kwenye Kinyanganyiro Baada Ya Kutishiwa Maisha,Kuchomewa Nyumba Zao, Simiyu Breaking News: Wagombea Wajiondoa Kwenye Kinyanganyiro Baada Ya Kutishiwa Maisha,Kuchomewa Nyumba Zao, Simiyu Reviewed by habari motto on 4:19 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.