Hali Tete Yatanda, Mabasi Yatekwa, Abiria Wakibwa Kila Kitu


Polisi wakiwa eneo la tukio.
Baadhi ya abiria waliotekwa.
“Walitushusha kwenye magari na kututaka tusalimishe kila kitu tulichokuwa nacho zikiwemo fedha na simu za mkononi. Waliokuwa wakionesha ukaidi walikuwa wakipigwa na kujeruhiwa vibaya,” alisema dereva mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Madereva hao waliendelea kueleza kuwa kazi hiyo ya utekaji iliendelea kwa takribani saa nzima ambapo kila gari lililokuwa likija eneo hilo, lilikuwa likitekwa na watu kulazimishwa kushuka chini na kutoa kila walichokuwa nacho.
Msichana huyu alizimia baada ya kutekwa.
“Walikuwa na mifuko mikubwa miwili, mmoja ulijaa simu walizotupora na mwingine ulijaa fedha, kwa kweli lilikuwa ni tukio baya sana, wengi walijeruhiwa vibaya,” alisema dereva mwingine ambaye naye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.
Abiria wengine waliozungumza na Uwazi, walienda mbele zaidi kwa kueleza kuwa mbali na kupigwa na kuporwa, pia baadhi ya abiria wanawake walibakwa na kusababishiwa maumivu makali.
“Huu unyama tuliyofanyiwa wa kupigwa na kuporwa mali zetu huku baadhi yetu wakibakwa unatisha sana na unaonesha ni kwa jinsi gani nchi inaelekea kubaya, hakuna amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya,” alisema mwanamke mmoja aliyekuwa miongoni mwa waliotekwa, aliyejitambulisha kwa jina moja la Sara.
Abiria hao waliliambia Uwazi kwamba eneo hilo lina pori kubwa ambapo panahitajika doria za mara kwa mara za polisi kwani ni eneo ambalo limekuwa maficho ya majambazi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino Mlowola alipopigiwa simu na kuulizwa juu ya tukio hilo, alikiri kuwa na taarifa na kueleza kuwa polisi walifika katika eneo la tukio muda mfupi baadaye baada ya kupata taarifa na kufungua barabara iliyokuwa imefungwa na kuruhusu magari kupita.“Msako mkali unaendelea kuwatafuta watuhumiwa katika Wilaya ya Kishapu na Kwimba,” alisema Kamanda Mlowola
Hali Tete Yatanda, Mabasi Yatekwa, Abiria Wakibwa Kila Kitu Hali Tete Yatanda, Mabasi Yatekwa, Abiria Wakibwa Kila Kitu Reviewed by habari motto on 8:33 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.