Hawa Ni Mastaa Wakubwa Waliompigia Saluti Diamond Platinum

BAADA ya Jumamosi iliyopita msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kunyakua tuzo tatu kwenye tuzo za Channel O zijulikanazo kama Channel O Africa Music Video Awards 2014 (CHOAMVA), zilizofanyika Afrika Kusini mwishoni mwa wiki iliyopita, mastaa mbalimbali nje na ndani ya nchi wamempigia saluti.
 

Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akipozi . 
Diamond ambaye ameweka rekodi nchini kwa kuwa msanii pekee kuchukua tuzo tatu kwa mpigo huku tuzo hizo zikiwa ni pamoja na ya Mwanamuziki Bora wa Kiume Afrika Mashariki, Video Bora ya Muziki wa Afro Pop, Mwanamuziki Bora Anayechipukia hivyo alikosa tuzo moja tu ya Video Bora kwa mwaka. 
Msanii mkali kutoka Nigeria Davido aliyetoa pongezi kwa ‘Diamond Platnumz’. Katika makala haya tunakuletea baadhi ya mastaa waliompigia saluti Diamond na kumpongeza kwa hatua aliyofikia.SUNDAY MANGU ‘LINEX’“Ukweli nampongeza sana Diamond na kikubwa nasema ametisha sana na ametutoa kimasomaso.”
DAVIDO

“Tanzania imesimama! Diamond Platnumz ameweza tena!” aliandika mwanamuziki huyu wa Nigeria kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram
Hawa Ni Mastaa Wakubwa Waliompigia Saluti Diamond Platinum Hawa Ni Mastaa Wakubwa Waliompigia Saluti Diamond Platinum Reviewed by habari motto on 9:54 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.