Jifunze Njia sahihi ya kubajeti Mshahara wako

Elimu ya hela na matumizi yake ni muhimu kuliko elimu nyingine yoyote kwa watu wanaofanya kazi za kuajiriwa, jambo la kusikitisha ni kwamba haifundishwi mashuleni na ni pasenti ndogo ya wazazi wanaofundisha watoto wao namna ya kutumia hela. Watu wanamaliza chuo kikuu, wanaanza kazi na bado wanaishia kukopa kwasababu ya kutokujua namna ya kubajeti matumizi.
100_7560 ED1[3]
Katika hii blog posti, utajifunza namna ya kupanga bajeti yako, namna ya kusavu hela na kusaidia ndugu zako. Watu wengi wanaishi maisha yasiyo na furaha kutokana na matumizi mabaya ya hela. Unakuta mtu anafanya kazi lakini anaishi mshahara kwa mshahara, huo ni utumwa.
Ukiangalia instagram utakuta watu wanafurahia mwisho wa mwezi ukifika, kisa? paycheck imeingia… Watu matajiri na waliofanikiwa kifedha,wanabajeti hela zao namna hii.
Asilimia 30% – inaenda kwenye kulipia kodi ya nyumba kwa walo wanaopangisha, au wanaojenga. Kama wewe tayari una nyumba, unaweza ukaweka asilimia 30 kwenye “investment” nyingine.
Asilimia 10 – inaenda kusaidia ngudu na wasiojiweza. Jinsi unavyotoa hela ndio jinsi zinavyoingia, hivi ndivyo dunia ilivyo.
Asimilia 10 inaenda kwenye savings account.
Asilimia 40 ndio ya matumizi yako ikiwemo chakula, usafiri, mavazi n.k.
Asilimia 10 inayobaki inaenda kwenye starehe “intertainment”.
Ukifuata hii formula, utajikuta muda wote una hela kwenye savings account kwa ajili ya emergency. Hamna haja ya kwenda kukopa, au kusubiri mwisho wa mwezi ili uende kutembea bagamoyo. Bagamoyo unaenda muda wowote kwani tayari umeshaweka fungu lake pembeni. Ukiishi kwa namna hii utakuwa na control na maisha yako na hutakuwa na matumizi makubwa kuliko kipato chako. Na kwasababu unaweka asilimia 10 kusaidia watu, utajikuta hela zinakurudia kwa namna ambavyo huwezi kuelezea.
Je wewe una unapangaje matumizi yako, acha komenti hapo chini.
Jifunze Njia sahihi ya kubajeti Mshahara wako Jifunze Njia sahihi ya kubajeti Mshahara wako Reviewed by habari motto on 9:25 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.