Muda uliopita ulikua ukizungumzia Wasanii wenye nguvu na waliofanikiwa kuupenyeza muziki wao kwenye nchi mbalimbali za Afrika ni lazima Wanigeria wataitawala hiyo list kama Iyanya,
Davido, Wizkid, P Square na wengine ila sasa Diamond anazidi kuipa Tanzania headlines
Video mpya ya staa wa Afrika Iyanya ya Mr. Oreo iliyotajwa na kituo cha TV cha TRACE Urban kama hit iliwekwa kwenye mtandao wa YouTube September 2014 ambapo mpaka December 15 ilikua imetazamwa zaidi ya mara milioni moja na elfu 80, huku Shekini ya P Square iliyowekwa November 20 kabla ya Diamond, ikiwa imetazamwa zaidi ya mara milioni moja laki moja lakini ya Diamond ambayo imewekwa November 20 2014 imetazamwa zaidi ya mara milioni moja na laki mbili.
Support ya Tanzania kwenye huu mwamko mpya wa kusupport vya nyumbani imechangia haya kwa kiasi kikubwa sana mpaka kumwezesha Diamond kushinda tuzo 3 za Channel O 2014, ushindi ambao ulifanya Wanigeria na wasanii wengine wa Afrika kujiuliza Diamond ni nani? kuanzia hapa ndio ikawa greenlight kwa Diamond.
Sasa hivi ni miongoni mwa mastaa wa Afrika wanaopata nafasi ya nyimbo zao kuchezwa sana kwenye TV mbalimbali za Afrika na hata kuwa kwenye level moja na mastaa wengine wakiwemo wa Nigeria ambao wametawala kwa kiasi kikubwa sana muziki wa Afrika.
Saa chache baada ya Diamond kushinda tuzo za Channel O Wasanii wa Nigeria na nchi nyingine za South Africa walivyokua wanamfata Diamond hotelini kwake na kuzungumza kuhusu kufanya kolabo, yani ni stori iliyogeuka manake zamani Diamond ndio alikua anahangaika kuwapata ili awashirikishe lakini sasa wao ndio wanamkimbilia yeye.
Kweli Diamond Plutnumz kiboko yao.
Reviewed by habari motto
on
7:48 AM
Rating: