Pinda kupingwa kwa maandamano Zanzibar

Bimani
Zanzibar. Vyama vya upinzani visiwani Zanzibar vimesema vitafanya kampeni ya kumshtaki Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa wananchi, iwapo hatojiuzulu kutokana na kashfa ya uchotaji wa Sh306 bilioni kupitia Akaunti ya Tegeta Escrow, ili kulinda misingi ya uwajibikaji wa pamoja.
Msimamo huo umetolewa na vyama vya CUF, TADEA na NCCR Mageuzi.
Mkurugenzi wa Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa CUF, Salim Bimani Abdalla alisema Waziri Mkuu ameonyesha udhaifu kwa kutochukua uamuzi wa kujiuzulu wadhifa wake ili kulinda misingi ya uwajibikaji wa pamoja.
Alisema CUF kitafanya maandamano nchi nzima kumshtaki Waziri Mkuu kwa wananchi kutokana na kitendo chake cha kuendelea kushika wadhifa, wakati fedha za umma zimepotea chini ya uongozi wake.
Makamu Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Zanzibar, Ambar Khamis Haji alisisitiza kuwa katika kuheshimu misingi ya utawala bora, Waziri Mkuu alitakiwa kujiuzulu badala ya kusubiri kuondolewa.
Alisema kwamba pamoja na Bunge kufanya kazi nzuri ya kufuatilia wizi huo, wabunge wameshindwa kumjadili Waziri Mkuu na kutoa mapendekezo, jambo ambalo limeleta doa katika kazi yao.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Tadea Zanzibar, Juma Ali Khatibu alisema: “Pinda alipaswa mwenyewe kufanya uamuzi mgumu wa kujiuzulu pamoja na kuwa hakuhusika moja kwa moja. Angefanya hivyo katika kulinda heshima yake na wananchi wapate muda wa kurejesha imani.”
mwananchi
Pinda kupingwa kwa maandamano Zanzibar Pinda kupingwa kwa maandamano Zanzibar Reviewed by habari motto on 1:43 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.