Mikoa ya mtwara na lindi iko hatarini kuingia gizani kutokana na kiwanda kilichopo msimbati kinachotumika kuchakata gesi inayotumika kufua umeme katika mikoa hiyo sehemu ya ardhi yake mita miamoja na sita, kumezwa na maji ya bahari na kubakia mita 25 kufika eneo la kiwanda.
Akizungumza na vyombo vya habari katika eneo la tukio naibu waziri nishati na madini mheshimiwa CHARLES KITWANGA amesema tukio hilo limetokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika nchi za malawi na msubiji na hivyo kuleta madhara upande wa tanzania.
Katika kukabiliana na hilo naibu waziri amelazimika kuitisha kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama na kuona njia rahisi ni kutumia jeshi la majini na nchi kavu ili kusaidia kuzuia sehemu ya kiwanda iliyobaki isimezwe na maji.
Huku muhandisi mkuu wa kiwanda hicho cha M and P PETER JOHN akisema endapo ardhi hiyo itaendelea kumegwa wakati wowote watasitisha kazi ili kunusuru maisha ya watu na mali zinazohamishika.
Mbali na kiwanda hicho pia bomba kuu la gesi linalotoka baharini na kuisafirisha gesi katika viwanda vya mtwara na lindi na hatimaye dar kinyerezi kwa ajili ya kufua umeme wa gredi ya taifa nalo liko hatarini kuadhirika kwani bahari imebakiza mita sita kufikia eneo la nchi kavu lilipo bomba hilo.
Dhoruba hiyo imetokea usiku wa tarehe 13 kuamkia tarehe 14 ambapo kipande cha ardhi chenye ukubwa wa mita miamoja na sita kiliweza kumezwa na maji ya bahari kwa muda wa masaa matatu.
LINDI NA MTWARA Hatarini Kuingia Gizani
Reviewed by habari motto
on
1:14 PM
Rating: