DESEMBA mwaka jana, mwezi ukiwa katikati kuna watu walipata bahati ya kuhudhuria mkutano wa waandishi wa habari ambapo moja ya wasambazaji wakubwa wa filamu nchin i Steps Entertainment walitangaza kushusha mauzo ya filamu zake kufikia buku jero yaani elfu moja na mia tano.
Katika mkutano huo walieleza sababu za kuamua kuuza filamu kwa bei hiyo.
Mwezi mmoja baadae serikali nayo ikasema zoezi lisimamishwe kwa kuwa linaonekana linaingilia kati mwenendo wa tasnia nchini.Lakini kingine kigumu sijui utakisemaje, mmoja wa wasanii machachari kabisa Steve Mengele “nyerere” amesema sinema kwenda buku jero ni laana.
Yeye alisema hayo wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Kanumba The Great Fallen huko landmark Hotel.
“Nasema tena filamu zetu kuuzwa buku Jero ni laana ya Kanumba, unafiki kutopendana ni Laana ya Adam Kuambiana, tumewaacha wenzetu waliotutangulia bila chochote,”
Msanii huyo alizidi kulalamika kuwa kuna watu waliwahi kusema kuwa yeye alikuwa chanzo cha ugomvi wa marehemu na kundi la Bongo movie lakini yeye ndio kafika katika uzinduzi lakini wale waliojifanya wema hakuna hata mmoja aliyefika katika uzinduzi wa kitabu cha Tree uliofanyika katika ukumbi wa Landmark Hotel.
Naam, hayo ndio maneno ambayo yanaweza kusababisha mazungumzo marefu na majadiliano ya kina miongoni mwa wadau wa sinema.
Wasambazaji wadogo wanaona kwamba kuuza kwa bei hii ni kuua tasnia.Lakini msambazjai huyu mkubwa anasema kwamba itasaidia sana kuondoa uharamia ambao umeshamiri sana nchini.
Pamoja na kauli hiyo kuna kauli za waziwazi kwamba moja ya wasambazaji wakubwa anafanya wizi na watu wanaukubali.
Filamu zinatengenezwaje?
Ilipoanza Bongo Movie kama masikhara, lakini waliochochea uwapo wa hiki kitu ni televisheni ambapo makundi ya kuigiza baadae yalijiingiza katika kutengeneza sinema ingawa hazikupendeza na kiwango lakini angalau mbuyu wa sasa ulianza kama mchicha tu na ilikuwa kazi sana kuuza VHS kwa watu watu walikaa katika luninga kuona michezo ya kuigiza iliyokuwa inaandaliwa na kundi la Kaole.
Nakumbuka sinema za Mwanzo na nakumbuka pia majadiliano yangu George Otieno al maarufu kama Tyson katika filamu yake ya Girl Friend iliyozinduliwa kwa mbwembwe, nakumbuka sinema ya Kibuyu ya Hammie Rajab, sinema zilizotoa sura fulani ya ugumu wa utengenezaji wa sinema hapa nchini.
Sikuwa na shaka na sinema ya Hammie rajab kwani yeye kitaaluma alikuwa mtengeneza sinema na alishafanyakazi nyingi ambazo wakati huo niliziandikia makala mbalimbali.
Mzee Hammie sehemu kubwa ya filamu zake alitengeneza kwa kuomba fedha na zile sinema za elimu alifanikiwa kupata fedha kwa mashirika husika na elimu anayoitoa na hivyo sinema hizo kimsingi zikabaki yeye kuwa dairekta na projuza wakati Projuza Mtendaji (mwenye hela) anabaki kama mwenye mamlaka. Kibuyu ilidhaminiwa na NSSF.
Katika miaka hiyo waliibuka wasambazaji wenye nguvu ambao pia walisambaza muziki Wananchi. Taratibu ikaja kampuni ya Steps baada ya hapo yamekuja makampuni mengine madogo yakifanya usambazaji. Na sasa zipo Sas O entertainment, Kapico Tanzania, Papazi entertainment na Pilipili Entertainment
Lakini kiukweli wakali wote unaowajua leo katika tasnia hii wanafanyakazi na Steps Entertainment. Hii ni moja ya kampuni ambayo imesaidia sana kusukuma tasnia ya filamu nchini hapa. Kampuni hii pamoja na kusambaza sinema , bali pia ilianza kuwa executive producer ikitoa fedha kwa skripti mbalimbali na hivyo kimantiki kumiliki sinema hizo.
Uharamia
Moja ya vitu vinavyoleta shida kubwa katika tasnia ya burudani nchini, ni uharamia wa sinema.Uharamia ni ile hali ya bidhaa za filamu kuwa katika soko bila ridhaa ya wahusika.
Kwangu mimi anayelamba hasara hii mmiliki wa sinema ambaye ni projuza mtendaji ambaye ndiye anayetoa hela za kufanyia kazi skripti.
Uhalifu huu unaofanyika Tanzania unatokana na sababu nyingi lakini kibaya zaidi ni kwamba sheria inayobana haki miliki bado kueleweka vyema hata kwa watengenezaji wenyewe ambao hata saundi traki zake si zao.
Juhudi zinafanyika kuondoa hilo tatizo pamoja na uwekaji wa alama lakini mambo yanaonekana kuwa bado mabaya.
Kwangu mimi naona hilo linatokana na uchumi wan chi na mfumo wa kuingia katika DVD moja kwa moja badala ya DVD kuwa hatua ya mwisho baada ya thieta na kufungua duka la vitu vilivyotumika kutengeneza sinema.
Kutokana na uchumi kuw amdogo na kwenda moja kwa moja katika DVD ni dhahrii uharamia utakuwepo kwani uwezo wa kuuza na kununua upo ndani ya raha ya watazama sinema ambao hawana nguvu kubwa kiuchumi.
Maamuzi ya Steps
Steps Entertainment Ltd ambayo ilianzishwa mwaka 2007 imekuwa mdau mkubwa katika kukuza tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa kutoa ajira nyingi kwa wadau mbalimbali wa tasnia ya filamu, wakiwemo waandaaji wa filamu Waigizaji, Wasambazaji wakubwa kwa wadogo, Wauzaji wa rejareja.
Ameweza kufanya hivi kwa kuwa anatoa fedha zake kuwapa maprojuza, kununua bidhaa zao na kuzisambaza mpaka nchi za nje.
Kutokana na kukithiri kwa uharamia wa filamu za Kitanzania na kuuzwa kwa bei ya chini mno, ambapo wananchi tumeweza kuzinunua kwa wingi kutokana na kuwa ni za bei rahisi sana. Maamuzi ya Steps ya kujaribu kupunguza bei za filamu zake ili kuona kama inaweza kusaidia kupunguza uharamia wa filamu hizi kuna mantiki.
Kuna ukweli wa wazo hilo kwani kama bidhaa ya uharamia ni buku buku na ninaenda kununua kuuziwa original buku jero siwezi kuenda kwa uharamia.
Mimi ninaamini Kampuni ya Steps Entertainment ltd ilifanya utafiti ili kujua ni jinsi gani filamu zinatoka mbali nje ya nchi zinawafikia walaji kwa bei ya chini sana .
Ikiwa tayari ina mtambo mkubwa wa kisasa wa kutengeneza cd/dvd na kuzirekodi hapa hapa nchini tofauti na siku za nyuma kupunguza bei za filamu zake ni muonekano wa kibiashara zaidi hasa ikizingatiwa kwamba yenyewe ndiyo inayotoa fedha za kutengeneza sinema.
Manufaa yapo
Uharamia umesababisha watu kama Steps ambao wao sit u wanazingatia filamu lakini marejesho ya fedha inazowekeza kubuni njia hii.
Suala hili linaweza kuwa na manufaa kwa wanaotaka kuona sinema, na hii itataka anayeingia katika fani pia kuwa bora ili aweze kumpata anayefaa kumsambazia sinema.
Akiwa mlipaji kodi mkubwa hainipi shida kuona mantiki ya Steps na kuacha kuangalia wasambazaji wadogo wanaofikiria elfu tatu ndio malipo halali wakati tunajua sote kwamba kinyume na kiwanda cha Steps huwezi kuuza bei hiyo kluna gharama zake.
Hodhi kubwa aliyonayo Steps huwezi ukaidharau, kwani maprojuza wakubwa wapo chini yake kwa kumkubali yeye kuwa Executive Producer na kumuondoa katika biashara ni kusababisha kuyumba ikizingatiwa kwamba serikali haifanyi biashara kazi yake ni kukusanya kodi.
Shida yetu nini
Mimi nafikiri shida ya tasnia hii ni mikataba ambayo haina maslahi makubwa na waigizaji na maprojuza wao.
Hili linawezekana kwa mfumo wa mikopo kubadilika katika mabenki na kuanza kutoa fedha kwa ajili ya watengeneza sinema. Nataka kusema hali ya kumtegemea mtu mmoja nayo inaleta uwiano mbovu wa maslahi lakini wigo wa kupata fedha za kazi ukitanuka itakuwa bora zaidi.
Kuongeza uwezo utasaidia kuwa na sinema bora yaani miradi inayotoa filamu zenye kusisimua ili makampuni yanayotengeneza sinema kuwa na uwezo zaidi wa malipo na kujiendesha.
Tatizo jingine ni watanzania kujipambanua zaidi na DVD badala ya kwenda thieta . Theita husaidia mauzo na kama wakianza kwenda thieta kama zamani fedha kwa wasanii wetu zitaongezeka.
Lakini ukiwa na maduka 79 pale Kariakoo na 9 tu ndio wanaouza sinema za kitanzania unahitaji mfumo unaofikiriwa na steps ili usifilisike.
mwisho
Filamu kwenda 'Buku Jero' ni kizunguzungu cha ukweli
Reviewed by habari motto
on
6:32 PM
Rating: