Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria ametembelea mji wa Baga ambao miezi miwili iliyopita ulishuhudia mauaji ya umati yaliyofanywa na wanamgambo wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram dhidi ya wakazi wa mji huo.
Katika ziara hiyo ya ghafla rais huyo amezungumza na wakazi na kuahidi kurejesha amani ya kudumu katika eneo hilo. Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria amewambia waandishi wa habari kwamba, safari yake katika mji huo ilikuwa na lengo la kuangalia hali ya mambo kwa karibu.
Huku zikiwa zimesalia wiki chache kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini Nigeria, rais huyo anafanya kila njama kuhakikisha anasalia madarakani ikiwemo kushadidisha mashambulizi dhidi ya kundi hilo la Boko Haram ambalo kwa miaka kadhaa limekuwa likitekeleza jinai mbalimbali dhidi ya raia wa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo bila kuchukuliwa hatua zozote za maana.
Aidha hivi karibuni Rais Jonathan aliwahakikishia wananchi wa taifa hilo hususan wakazi wa majimbo yaliyoko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo kwamba, muda si mrefu, siku za maombolezo kwa ajili ya watu wao wanaouwawa kutokana na mashambulio ya kundi la Boko Haram zitafikia tamati.
Rais wa Nigeria azuru mji uliokombolewa wa Baga.
Reviewed by habari motto
on
11:09 AM
Rating: