Tukio hilo lilitokea jana saa saba mchana katika kijiji cha Bulyaheke, kata Bulyaheke, baada ya wananchi kumkamata mtuhumiwa huyo katika kijiji cha Kazunzu na kuwaongoza hadi kijiji cha Bulyaheke kwa mganga huyo.
Wananchi wa vitongoji vya Kazunzu, kijiji cha Nyambemba, kata ya Kazunzu, wakishirikiana na wa kitongoji cha Lueseselo, kata ya Bulyaheke, wamempiga kwa marungu, mawe na mapanga na kisha kumchoma moto mtu ambaye bado hajafahamika, wakimtuhumu kuwa wakala wa kuteka watoto wakiwamo walemavu wa ngozi (albino), akishirikiana na waganga wa kienyeji wapiga ramli kwa imani za kishirikina za kupata utajiri.
Mbali ya kumuua, wananchi hao pia wamevunja na kuchoma moto nyumba 13 zilizoezekwa kwa bati mali ya mganga wa kienyeji mwanamke mpiga ramli mwenye umri wa miaka 40 (jina linahifadhiwa).
Hata hivyo, mganga huyo na familia yake walifanikiwa kuwatoroka wananchi hao.
Tukio hilo lilitokea jana saa saba mchana katika kijiji cha Bulyaheke, kata Bulyaheke, baada ya wananchi kumkamata mtuhumiwa huyo katika kijiji cha Kazunzu na kuwaongoza hadi kijiji cha Bulyaheke kwa mganga huyo.
Richard Mangalamu baba wa mwanafunzi aliyetekwa, Winfrida (11) anayesoma darasa la nne Shule ya Msingi Kazunzu, alisema mtuhumiwa alimwachia mwanafunzi huyo kutokana na kumkuta ana chale mgongoni na kifuani akidai amepoteza ubora.
Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Wilaya ya Sengerema, Babu Sanare na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Enock Mabula, kwa nyakati tofauti walithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Naye Diwani wa Bulyaheke, Bagadi Nyuki, akiwa eneo la tukio, alisema chanzo cha mauaji hayo ni marehemu kudaiwa kuwa juzi alimteka mwanafunzi wa kike anayesoma darasa la nne katika Shule ya Msingi Kazunzu na kumvutia vichakani na kisha kumvua nguo na kumpapasa.
Inadaiwa kuwa alimuachia huru baada ya kugundua kuwa hakuwa na sifa zinazohitajika na mganga na mwanafunzi huyo alipofika nyumbani aliwaeleza wazazi wake na ndipo wakishirikiana na wanakijiji wenzao walianza kumsaka mtuhumiwa na kufanikiwa kumtambua.
Inadaiwa baada ya kubanwa mtuhumiwa huyo alikiri na kujitambulisha alikuwa ametoka kijiji cha Katoro, mkoani Geita na alikwenda Sengerema kwa kazi ya uwakala wa kuteka watoto.
Insurance
Diwani huyo alisema marehemu aliomba apelekwe kijiji jirani cha Bulyaheke umbali wa kilometa sita kutoka Kazunzu kwa mwenyeji wake na mdau mwenzake, Sato, lakini wapofika walikuta amekwisha kutoroka.
Wakati huohuo, mwili wa mtoto Yohana Bahati aliyeuawa kwa kukatwa miguu na mikono, mwili wake utazikwa kesho katika kijiji cha Kataro, mkoani Geita.
CHANZO NIPASHE
Wakala Wa Kuua Albino Auawa Kwa Moto
Reviewed by habari motto
on
8:30 AM
Rating: