Watu watatu wamefariki dunia kwa ajali ya moto akiwemo utingo wa gari hilo aliyefia hospitari kwa kuvuja damu nyingi na watu kumi na nne kujeruhiwa na kulazwa katika hospitari ya Igogwe na watutu kuthibitishwa na Dactari kuwa hali zao ni mbaya baaada ya gari aina ya scania lenye namba za usajiri T821ARF mali ya kampuni ya Ilasi likiwa limebeba mafuta ya petrol, kuacha njia na kupinduka mida ya saa tatu usiku eneo la kijiji cha Isongole (namber one ) kata ya Isionje . Moto huo uliosababishwa na mwanamke aliekuwa na kibatari kwenda kumulika mafuta katika mfereji wa maji uliopo eneo la tukio kwa kibatari chake ili ajue kama yale ni mafuta au maji kitendo kilichosababisa moto kuwaka kufuata mafuta yaliyo kuwa yakimwagika mpaka eneo gari lilipoanguka hivyo kusababisha watu mifugo na mashamba kushika moto. Moja wa shuhuda wa tukio aliyejitambulisha kwa jina moja la Matola amesema kwamba gari lilianguka mida ya saa tatu usiku ndipo wananchi walikimbilia kuchota mafuta na dereva na baabhi ya wakazi aliwaktaza kusogea eneo hilo na kuwataka wawasaidie kutoka eneo hilo na baada ya mda kidogo wao kutolewa ndipo moto ulilipuka kutoka katika mfereji wa maji na kusambaa kufuata mafuta yalipo hadi kufika kwenye gari. Bwana Matola alifafanua kuwa“ Tunashukuru moto uliwahi kuwaka kabla ya watu kujaa hata hivyo baadhi ya wenyeji wa eneo hilo walijitahidi kuzuia watu wasichote mafuta lakini wengine hawakuweza kuwasikiliza wakizani kwamba watapata mafuta kama ilivokuwa juzi (siku tatu nyuma )baadaya gari la mafuta ya dizeli kuanguka na wao kuchota mafuta mengi na kuuza lita ishirini kwa shilingi elfusaba tu, hadi alipotokea mama moja ambae ni moja wa waliofariki kuja na kibatari kumulika mferejini ili kujua kama yale ni mafuta au maji na ndipo mafuta yakashika moto.” Dereva wa gari hilo Zawadi nyato aliyekimbizwa hospitali ya igogwe baada ya kupata ajari amesema kuwa alipokuwa kwenye mlima anashuka taa ya upepo iliwaka kuashiria hakuna upepo na kwa sababu alikuwa amebeba mzigo mzito gari likamshinda na kujikuta yuko hospitalibila kujua kilichoendelea hapo. Nae mkuu wa wilaya Mhe. Chrispin meela amefika eneo la tukio kutoa pole na lambi rambi kwa wakazi wa eneo hilo na kuwakumbusha kuwa wawe makini na vitu vya hatari kama hivi kwani tukio kama hili liliwahi kutokea katika mtaa huo huo na kusababisah vifo vya watu wengi lakini bado wanarudia kitendo kama hicho. Hivyo amewataka watu wabadilike na wajifunze kupitia matukio yaliyopita. Ajari ya moto kama hii iliwahi kutokea miaka ya 1990s katika kata hiyohiyo ya Isionje mtaa wa numba one mita chache kutoka ilipotokea ajali hii ya leo na kuuwa watu wengi waliozikwa kwa pamoja katika eneo hilo kwani walishindwa kutambulika na ndugu zao na kijeruhi mamia ya watu. Kwa hisani ya TUMAIN OBEL KINGO TANZANIA Rungwe
Watu 3 wafariki dunia kwa ajali ya moto
Reviewed by habari motto
on
10:15 AM
Rating: