Baadhi ya majirani wa mtaa wa Hayanga RRM jijini Mbeya wakiwa nje ya nyumba ambapo tukio hilo limetokea .
Waombolezaji
Watu wawili wafanyakazi shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Mbeya Ndugu Uswege Mwankuge (58) na Jusio Uswege (48) ambao ni mtu na mke wake wamekutwa wamekufa ndani ya nyumba yao mtaa hayanga RRM jijini mbeya .
Tukio hilo la kusikitisha limetokea leo jijini hapa ambapo inadaiwa kuwa wawili hao wamekutwa wamekufa ndani ya nyumba yao usiku wa kuamkia leo Marchi 3 mwaka huu
Akizungumiza tukio hilo Balozi wa mtaa huo Jofrey Katuli amesema yeye alipigiwa simu majira ya saa 4 asubuhi kuwa Ndugu Uswege Mwankuge pamoja na mke wake ndugu Jusio Uswege wamekufa wakiwa ndani ya nyumba yao .
Amesema watoto wa marehemu ndio waliogundua kuwepo kuwepo kwa tukio hilo kutokana kuwepo kwa ukimywa wa muda mrefu ndani ya chumba cha wazazi wao ambapo walilazimika kuingia chumbani na kumkuta baba na mama yao tayari wakiwa wamekufa .
Amesema baada ya kugonga kwa muda mrefu bila kufunguliwa walilazimika kubomoa mlango ambapo walikuta baba yao akiwa amening'inia juu huku tayari akiwa amekufa kwa kujinyonga ambapo mama naye alikuwa amelala kitandani huku akiwa amekwisha fariki ambapo mwili wake ukiwa na majeraha sehemu za usoni.
Amesema baada ya kupata maelezo hayo walipiga simu kituo cha Polisi ambapo walifika na kuchukua miili ya watu hao na kuipelekea hospital ya rufaa Mbeya kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kwa mujibu wa balozi huyo amedai kuwa inawezekana kuwa mwanaume huyo ambaye sasa ni marehemu alimuua mke wake kwa kumpiga na kitu kizito kichwani hadi kufa kuku yeye akijaribu kujiua kwa kutumia sumu ambayo ilishindikana na kutumia mbinu ya kujinyonga ambayo aklifanikiwa nayo.
Mmoja wa Majirani wa marehemu hao Ndugu Alex Kyabyara amesema hawakuwahi kusikia ugomvi wa aina yeyote baina ya wawili hao hivyo tukio hilo limewastaajabisha huku wakishindwa kujua nini chanzo cha mauji hayo.
Akithibisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa mbeya Ahmed Msangi amesema tukio hilo limetokea majira ya saa Nne asubuhi ambapo amedai kuwa watu hao walikuwa na ungomvi usiku wa manane hali ambayo imepelekea mauiji hayo.
Aidha kamanda msangi amekili kuwa wawili hao ambao ni mke na mume bado walikuwa ni watumishi wa shirika la umeme tanesco mkoa wa mbeya hadi umauti huo unawakuta.
Amesema bado uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika ili kubaini chanzo cha mauiji hayo ambapo miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika hospital ya rufaa jijini Mbeya.
NA JAMIIMOJA BLOG
Wakutwa Wamekufa Ndani Ya Chumba Cha Kulala
Reviewed by habari motto
on
1:05 PM
Rating: