Mtangazaji gwiji wa soka, wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC, Charles Hillary Nkwanga, akizungumza katika hafla ya kumuaga kwenye studio za radio hiyo zilizoko London Uingereza. Kwa mujibu wa habari zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii hapa nchini, Nkwanga, anatua Bongo leo jioni Aprili 3, 2015 tayari kujiunga na kituo cha televisheni cha Azam TV, cha jijini Dar es Salaam, kinachomilikiwa na tajiri wa kitanzania, Said Salim Bakhresa. Tayari Bakhresa ameshamchukua mtangazaji mwingine nguli wa BBC, Baruani Mhuza aliyekuwa akifanyia kazi kutoka hapa Dar es Salaam. Kabla ya kujiunga na BBC, Charles Hillary alikuwa mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani Deutchewelle, ambako alitangaza kwa miaka mingi akitokea radio ya kwanza ya FM, Radion One Sterio. Kabla ya kujiunga na Radion One Sterion, Charles Hillary, kipande cha mwanaume, alikuwa mtangazaji wa Redion Tanzania Dar es Salaam (RTD), hivi sasa TBC. Umaarufu wa mtangazaji huo unatokana na umahiri wake wa kutangaza kabumbu, weengine wakiita soka lakini kwa kiswahili cha kawaida, mpira wa miguu, ambapo sauti yake nzito huwavutia wasikilazi wengi hususan wale wa soka. Katiba BBR Charles Hillary alikuwa mtangazaji wa kutumainiwa wa soka ya ligi kuu ya Uingereza.
Charles Hillary akipewa zawadi ya jezi nyekundu yenye jina lake na mhariri wa idhaa ya kiswahili ya BBC, Ali Saleh, (katikati), na mtangazaji mwenzake, Peter Musembi
Reviewed by habari motto
on
1:43 PM
Rating: