1.Tulia kisha lala chini. Ukikimbia bomu likilipuka ni rahisi kukumbana nalo unakokwenda.
2.Pumua taratibu ili usikose hewa kutokana na hewa nzito ikiwa shambulio ni bomu.
3.Tambaa taratibu ukiwa umeinama hadi sehemu yenye kitu ambacho hakitikisiki.
4.Usikae karibu na vitu vya kuvunjika kama madirisha au kabati la vioo na vifaa vya umeme.
5.Ikiwa waokoaji wamefika katika eneo la tukio hakikisha unafuata maelekezo yao .
6.Katika tukio kama hilo unakumbushwa kuwasaidia watu wenye ulemavu.
7.Ukiwa unatoa msaada kwa wahanga wenzako, usimguse mtu aliyejeruhiwa.
8.Usikae karibu na jiko au kifaa chenye gesi kwa sababu inaweza kulipuka.
9.Ukifanikiwa kutoka ndani ya jengo, kaa mbali nalo, linaweza kukudondokea.
10.Kama ulikuwa ghorofani usitumie ‘lift’ tumia ngazi.
Reviewed by habari motto
on
10:25 AM
Rating: