Man City Yapigwa 2-1



Manchester City imeshindwa kutumia vema kiporo chake dhidi ya Crystal Palace na kujikuta ikitandikwa bao 2-1. Kwa matokeo hayo, Manchester City sasa imekaa rasmi chini ya Manchester United ambayo iko nafasi tatu kwenye msimamo wa Ligi kuu kwa pointi zake 62 dhidi ya 61 za City inayopumua kwenye nafasi ya nne. Timu zote (ukiondoa Chelsea na Leicester City zenye michezo 30) zimecheza michezo 31.

 Hadi mapumziko Crystal Palace ilikuwa mbele kwa bao moja lililofungwa na Glenn Murray katika dakika ya 34. Dakika ya 48 Palace wakaongeza bao la pili kupitia kwa Jason Puncheon kabla Yaya Toure hajaifungia City bao la kufutia machozi dakika ya 78. United na City zinakutana Jumapili hii katika mchezo wa kufa na kupona.
Man City Yapigwa 2-1 Man City Yapigwa 2-1 Reviewed by habari motto on 8:01 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.