Ndege Ya Ufaransa Nusura Kupigwa Kombora La Korea Kaskazini


Ndege moja ya Ufaransa iliokuwa na abiria 330 ilikuwa kilomita 100 pekee na kombora la masafa marefu lililorushwa na Korea Kaskazini maafisa wanasema.

Ndege hiyo ilipita katika eneo ambalo kombora hilo lilinguka dakika 10 baadaye.

Kampuni ya Airfrance inasema kuwa ndege yake haikuwa hatarini lakini imejiweke marufuku ya kusafiri katika anga ya Korea Kaskazini kama tahadhari.
Pentagon inasema kuwa kombora hilo lilipaa katika anga yenye shughuli nyingi.

Maafisa wa Marekani mara kwa mara wamekuwa wakionya kuhusu hatari zinazoletwa na makombora dhidi ya ndege za abiria katika eneo hilo. Kombora la masafa marefu ICBM 

Njia iliotumiwa na ndege hiyo aina ya Boeing 777 inaonyesha kuwa ilikuwa magharibi, mwa Hokkaido, kaskazini mwa taifa la Japan , wakati bora hilo la Korea Kaskazini lilikuwa hewani.

Japan na Marekani inakadiria kwamba kombora hilo lilianguaka kati ya kilomita 100na 150 karibu na ndege hiyo.

"Kombora hilo liliruka katika anga na kuanguka nchini Japan, eneo ambalo hutumika na vyombo vya kibiashara na vile vya uvuvi , msemaji wa Pentagon Jeff Davis alisema


Credit kwa 

Juma Mtanda wa jumamtanda.blogspot.com

Ndege Ya Ufaransa Nusura Kupigwa Kombora La Korea Kaskazini Ndege Ya Ufaransa Nusura Kupigwa Kombora La Korea Kaskazini Reviewed by habari motto on 7:02 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.