Shibuda amlilia Chipaka


Kifo cha muasisi wa Ada-Tadea (zamani Tadea), John Lifa Chipaka kimeacha pigo ndani ya chama hicho, huku katibu mkuu wake, John Shibuda akidai kuwa mwanasiasa huyo aliwaunganisha wanachama na kuwatetea wayonge.
Tadea ambayo iliasisiwa na mwanasiasa wa zamani, Oscar Kambona ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali katika utawala wa awamu ya kwanza kabla ya kukimbilia uhamishoni London, Uingereza baada ya kuhitilafiana na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kwa miaka mingi ilikuwa chini ya Chipaka.
Mwanasiasa huyo ambaye aliwahi kujitosa kuwania urais, lakini akaenguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) anazikwa kesho jijini Dar es Saalam.
Shibuda alisema jana kuwa, chama chao kimepoteza mtu muhimu aliyewaunganisha na kwamba, msiba wa mwanasiasa huyo upo Mikocheni karibu na Barabara ya Warioba.
Katibu huyo alisema kwamba maandalizi ya mazishi yanaendelea.
Chipaka alifariki dunia juzi katika Hospitali ya Ibrahim Haji akiwa na miaka 80.
Mpaka anakumbwa na mauti alikuwa mwenyekiti wa chama hicho ambacho awali kilifahamika kama Tadea. Alifariki kutokana na shambulio la moyo.
Mwanasiasa huyo alikuwa miongoni mwa wajumbe walioshiriki Bunge Maalumu la Katiba mwaka 2015 na chama chake kilikuwa kati ya vyama vichache vya upinzani vilivyoshiriki uchaguzi wa marudio wa Zanzibar mwaka 2016 baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa awali.

Credit kwa George Njogopa, Mwananchi gnjogopa@mwananchi.co.tz
Shibuda amlilia Chipaka Shibuda amlilia Chipaka Reviewed by habari motto on 11:43 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.