Mo Salah achunguzwa


Haki miliki ya picha

Related image
Mshambuliaji wa Liverpool raia wa Misri Mohamed Salah anachunguzwa na polisi baada ya video yake kuibuka akionekana kuendesha gari akiwa bado anatumia simu.
Klabu yake inadaiwa kuwa ndiyo iliyopiga simu kwa polisi.
Polisi wa Merseyside wamethibitisha kupitia ujumbe wa Twitter kwamba video hiyo imekabidhiwa kitengo husika.
Msemaji wa Liverpool amesema waliwafahamisha polisi kuhusu video hiyo baada ya kuzungumza na mchezaji huyo
Ameongeza kwamba hatua zozote zinazohitajia kuchukuliwa kuhusu tukio hilo zitachukuliwa kwa kufuata mifumo ya ndani.
Video hiyo ambayo imesambazwa sana kwenye Twitter inaonekana kumuonesha mchezaji huyo, akiwa anatumia simu yake akiwa amelisimamisha kwa muda huku akiwa amezingirwa na mashabiki, wakiwemo watoto. Kisha analingurumisha gari na kundoka akiwa bado anaitumia simu yake.

SalahHaki miliki ya picha
Image captionVideo hiyo inayodaiwa kumuonesha Mo Salah akiendesha gari akiwa bado anatumia simu imesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii

Msemaji wa klabu hiyo amesema: "Klabu, baada ya kushauriana na mchezaji, imewafahamisha Polisi wa Merseyside kuhusu kanda hiyo ya video na matukio yaliyokuwa yanaendelea wakati wa kupigwa kwa video hiyo."
"Tumezungumza na mchezaji huyo na tutashughulikia hatua nyingine zozote zinazohitajika kuchukuliwa kwa kutumia mifumo ya ndani.
"Hakuna yeyote kati ya klabu na mchezaji ambaye atatoa taarifa zaidi kuhusu tukio hili."
Raia huyo wa Misri aliwafungia Liverpool magoli 44 msimu uliopita.
Mo Salah alifunga bao Jumapili katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England msimu huu ambapo aliwasaidia Liverpool kuwalaza West Ham 4-0.
Mabao hayo mengine yalifungwa na Sadio Mane (mawili) na Daniel Sturridge.
Mo Salah achunguzwa Mo Salah achunguzwa Reviewed by habari motto on 7:02 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.