Waliofariki Kwa Corona Marekani Wafika 12,722

Marekani imerekodi vifo vingi vya ugonjwa wa corona kwa siku huku watu 1,736 wakifariki siku ya Jumanne.

Idadi hiyo inaweka watu waliofariki kutokana na virusi hivyo nchini humo kufikia 12,722 kulingana na data za chuo kikuu cha Johns Hopkins.
Marekani ina wagonjwa 398,000 wa virusi hivyo waliothibitishwa , ikiwa ndio idadi kubwa zaidi duniani .
Wakati hayo yakijiri, Rais wa Marekani Trump ametishia kulikatia fedha shirika la afya Duniani WHO kwa sababu amesema shirika hilo halikutilia maanani kwa namna ilivyopasa hatari ya maambukizi ya virusi vya corona.
Trump amelilaumu shirika hilo kwa kuegemea zaidi upande wa China.  Rais huyo wa Marekani amedai kwamba asasi hiyo ya kimataifa ilishirikiana na China katika miezi kadhaa iliyopita kupuuza hatari ya maambukizi ya virusi vya corona.
Akitoa taarifa juu ya hali ya maambukizi hayo nchini Marekani, Trump alipuuza umuhimu wa taarifa ya mshauri mwandamizi iliyotolewa mapema mwaka huu kutahadharisha juu ya uwezekano wa kulipuka kwa maambukizi hayo. Rais huyo amedai kwamba hakuiona taarifa hiyo.
Badala yake Rais huyo wa Marekani amelishukia shirika la afya duniani WHO na kulitishia kulikatia fedha.Trump amesema asasi hiyo inaegemea sana upande wa China kuhusu mkakati wake wa kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.
Amedai kwamba Shirika la WHO lilishirikiana na China katika juhudi za nchi hiyo za kupunguza hatari ya mlipuko wa maambukizi hayo.
Rais Trump amesema Shirika hilo limeisifu China ingawa pana sababu ya kuwa na mashaka juu ya idadi rasmi  iliyotolewa na serikali ya China juu ya vifo vilivyotokana na mambukizi ya virusi vya corona
Waliofariki Kwa Corona Marekani Wafika 12,722 Waliofariki Kwa Corona Marekani Wafika 12,722 Reviewed by habari motto on 10:33 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.