Mazishi ya Rais Sata yasimamishwa kwa muda

TARARATIBU za kumuaga rais wa Zambia, Michael Sata , zimesimamishwa kwa muda hadi mchana leo.
Akitoa maelekezo hayo kwa umma Katibu wa Baraza la Mawaziri, Rowland Msiska  hakutoa sababu za kusimamishwa kwa shughuli ya kumuaga rais huyo aliyefariki London Oktoba 28 mwaka huu katika hospitali ya King Edward VII .
Kwa kauli hiyo utoaji salamu za mwisho hautafanyika asubuhi ya leo hadi mchana sana.
Hata hivyo katibu huyo alisema kwamba watu wataendelea na shughuli hiyo ya mazishi Jumapili, ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kutoa salamu za mwisho.
Rais huyo anatarajiwa kuzikwa Jumanne Novemba 11 mwaka huu katika viwanja vya Embassy mjini Lusaka.
Wakati huo huo mamlaka ya Jiji la Lusaka limesema kwamba barabara nyingi zitafungwa Jumatatu na Jumanne ili kuruhusu shughuli za mazishi na maziko kufanyika.
Kwa mujibu w ataarifa hizo karibu nusu ya barabara muhimu za jiji hilo zitafungwa kwa muda.
Tangazo kwa madereva limesema kwamba barabara hjizo zitafungwa kuanzia  saa 12 na nusu asubuhi hadi saa saba na nusu mchana kwa siku zote mbili.
Barabara ziotazofungwa ni:
 • Great East Road
• Great North Road
• Church Road
• Cairo Road
• Addis Ababa road
• Chikwa Road
•Independence Avenue
• Pundit Neru
• Haile Salassie
• Nationalist Road
Mazishi ya Rais Sata yasimamishwa kwa muda Mazishi ya Rais Sata yasimamishwa kwa muda Reviewed by habari motto on 1:51 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.