Chelsea bado inaongoza ligi

London, England. Kocha Jose Mourinho anaamini kuwa kuna kampeni chafu ya kuchanganya uamuzi dhidi ya Chelsea katika michezo yake.
Mourinho alikuwa mwenye hasira dhidi ya mwamuzi Anthony Taylor aliyeshindwa kuipa timu yake penalti wakati wa mchezo ulioisha kwa sare ya bao 1-1 na Southampton juzi.
Kiungo Cesc Fabregas alionyeshwa kadi ya njano kwa kudaiwa kujiangusha ndani ya eneo la hatari baada ya kugongana na Matt Targett.
Baada ya mchezo huo, Mourinho aliiambia BBC Sport akisema: “Vyombo vya habari, watangazaji wa mechi, makocha wa timu nyingine wote wanafanya kazi ya kuwapa presha waamuzi.”
Katika mkutano wake na waandishi wa habari baadaye, aliongeza: “Kuna kampeni inafanywa dhidi ya Chelsea. Sijui ni kwa nini hili linafanyika, lakini sitajali.
“Kila mtu anajua kuwa ilikuwa ni penalti. Mwamuzi alifanya makosa, watu wanafanya makosa lakini alifanya kosa kubwa.
“Ni mwamuzi mzuri na mtu mzuri, ni kijana mdogo, ana miaka mingi ijayo katika soka lakini alilofanya ni kosa kubwa.”
Mwamuzi Taylor alimhukumu Fabregas kuwa aliyejirusha baada ya kukabwa na Targett, lakini picha zinaonyesha kuwa kulikuwa na aina ya mgongano katika tukio hilo uliofanywa na beki huyo mwenye miaka 19.
Fabregas, ambaye alilalamikia uamuzi wa kunyimwa penalti, alisema: “Bila shaka kulikuwa na kugongana. Mwamuzi hakuchezesha vizuri na sidhani kama atalala vizuri. Alikuwa na mchezo mbovu.”
Kocha wake, Mourinho alisema awali kuwa presha kutoka kwa vyombo vya habari vilisababisha Chelsea kunyimwa penalti katika kipindi cha pili cha mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa St Mary.
Kocha wa West Ham, Sam Allardyce alimshutumu Branislav Ivanovic kuwa alijiangusha kirahisi akisaka penalti katika mchezo ambao vigogo hao wa London walishinda kwa mabao 2-0 Ijumaa iliyopita.
Mourinho aliongeza kusema: “Baada ya mchezo dhidi ya West Ham, Sam alizungumza juu ya Branislav Ivanovic (kujiangusha). Hii ni nini? Tena, unakuja hapa (Southampton) unakutana na uamuzi mbaya na mwamuzi anashindwa kutenda haki. Amefanya kosa.
Chelsea bado inaongoza ligi Chelsea bado inaongoza ligi Reviewed by habari motto on 1:46 PM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.