Mwanaume mmoja kutoka Mpumalanga, Afrika Kusini amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkobola kwa kosa la kumuua mpenzi wake na kumzika katika bustani iliyo nyuma ya nyumba yake.
Tukio la kupotea kwa mwanamke huyo liliripotiwa katika kituo cha Polisi siku ya Jumapili January 4, siku iliyofuatia Polisi walianza na upelelezi wa tukio hilo, mwanaume huyo alihojiwa, alipoulizwa kuhusu mahali alipo mwanamke huyo ambaye alikuwa ni mpenzi wake, alijibu kwamba hajamuona kurudi nyumbani hapo tangu alipoaga kwenda kutoa pesa Benki.
Ukaguzi ulipokamilika ndani ya nyumba Polisi walihamia nje ya nyumba wakagundua kuna udongo unaoonyesha kuchimbwa siku za karibuni, alipoulizwa alichimba kwa ajili ya nini akasema alikuwa analima.
Polisi walitilia shaka maelezo yake, wakaagiza iletwe koleo ili wachimbe, jamaa huyo akakiri kwamba ni kweli kamuua mpenzi wake na kumzika katika bustani hiyo.
Amuuwa mpenzi wake na kumzika kwenye bustani ya mboga
Reviewed by habari motto
on
11:45 AM
Rating: