Azam FC wakorofisha Sudan

AZAM FC imekwenda Sudan ikiwa kamili na tayari kwa lolote katika kurudiana na El Merreikh kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika keshokutwa Jumamosi.
Pia katika kujiridhisha na mambo, wameamua kujipikia wenyewe msosi.
Azam wamepata msaada kutoka kwa wanafunzi wa Tanzania wanaosoma katika Chuo cha African University ambao wanawapa sapoti ya kila kitu.
Katibu Mkuu wa Azam, Nassor Idrissa, ameliambia Mwanaspoti akisema: “Huku tunafanya kila kitu wenyewe. Kuna wanafunzi wa Tanzania wanasoma huku wanatupa sapoti kubwa sana kwa kila kitu.”
Beki wa kati wa Azam, Aggrey Morris, amesema wanatarajia matokeo mazuri lakini ameomba Watanzania wawaombee dua kwani wanalitangaza jina la nchi.
Timu hiyo iliwasili Sudan juzi Jumanne usiki na kulikataa basi walilotayarishiwa na wenyeji wao.Insurance

Azam FC wakorofisha Sudan Azam FC wakorofisha  Sudan Reviewed by habari motto on 10:55 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.