Nyota Torres atua Ac Milan

Adios: Chelsea striker Fernando Torres has completed a permanent move to AC Milan on a two-year deal
HATIMAYE Fernando Torres amehitimisha miaka yake mitatu na nusu isiyo na mafanikio ndani ya Chelsea baada ya kukubali kujiunga na AC Milan.
Mshambuliaji huyo wa Hispania anakwenda kuziba pengo la Mario Balotelli aliyekwenda Liverpool kwa pauni milioni 16.
Wakala wa Torres alikamilisha mazungumzo na AC Milan kabla mchezaji wake kukubali kujiunga na timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.
Vyanzo vya habari nchini Italia vinasema Torres anakwenda AC Milan kama mchezaji huru na kilichobakia sasa ni mara kufuzu vipimo vya afya Jumamosi.
Torres aliyechemsha vibaya Chelsea na kuifungia mabao 45 tu katika mechi 172, alikuwa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake Stamford Bridge unaomwingizia pauni 150,000 kwa wiki.
Nyota Torres atua Ac Milan Nyota Torres atua Ac Milan Reviewed by habari motto on 2:40 AM Rating: 5
ads 728x90 B
Powered by Blogger.